Home »
» DKT. SHEIN AMTOLEA UVIVU MAALIM SEIF
DKT. SHEIN AMTOLEA UVIVU MAALIM SEIF
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraz a la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein,amesema kauli
zinazotolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hama d
juu ya mchakato wa Katiba Mpya hasa kwenye suala la Mu ungano ni maoni
yake binafsi si msimamo wa Serikali au Wazanzibari.
Alisema licha
ya Katiba kutoa uhuru wa kujieleza, hakuna kiongozi anayeweza kuwa na
uwezo wa kuw asemea wananchi wa Zanzibar katika mchakato wa Katiba hasa
kuhusu Muundo wa Serikali.
Dkt.Shein aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar
jana alipozun gumza na waandishi wa habari ili kuelezea maen deleo ya
Serikali katika kipindi cha miaka mitatu .
Aliongeza kuwa , kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kiongozi mwenye mamlaka ya kuwasemea Wazanzibar ni yeye pekee si vinginevyo.
Kauli
hiyo ya Dkt. Shein ,imekuja siku chache baada ya Maalim Seif kunukuliwa
na vyombo vya habari akitoa ms imamo wa Wazanzibari kuhusu Muundo wa
Muunga no na suala zima la kupigania mamlaka kamili ya Zanzibar na
kutaka Serikali tatu.
“Kila mtu kwenye Katiba ana haki ya kusema
lakini Maalim Seif hawezi kuisemea Serikali,anayosema kuhu su Muundo wa
Serikali ni maoni yake na chama chake, yeye si Msemaji wa Serikali, mimi
ndiyo msemaji,” alisema Dkt .Shein,baada ya kuulizwa msimamo wake
kuhusu kauli tata zinazotolewa na Maalim Seif.
Licha ya hali hiyo,
Dkt. Shein alisema katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hakuna tofauti
bali jambo la msingi ni kuvumiliana badala ya kila mtu kufanya
anavyotaka.
Akizungumzia mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu,
alisema maendeleo makubwa yamepatika na katika Nyanja
mbalimbali,kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya,maji na
miundombinu.
Matukio ya tindikali
Akizungumzia matukio ya
umwagiaji watu tindikali, Dkt. Shein alisema Serikali imekuwa ikichukua
hat ua mbalimbali za kukabiliana na wahalifu hao na kusisiti za kuwa,
kamwe hawatarudi nyuma kupambana na wahalifu hao.
Alisema matukio
hayo yalianza mwaka 199 5 ambapo kijana mmoja Mjini Wete, alimwagiwa
tindikali na kusisitiza kuwa, Serikali itaendelea kuwasaka na kuwafikis
ha katika vyombo vya sheria watu wote watakaojih usisha na vitendo
hivyo.
Suala la ubaguzi
Dkt. Shein alisema,vitendo vya kibaguzi
vinavyodai wa kufanywa na baadhi ya watu visiwani humo kutoa kauli za
kuwabagua wananchi wa Pemba, wanaofanya vitendo hivyo wakibainika ,
watachukuliwa hatua.
Alisema tayari ameviagiza vyombo vya dola
kufuatilia nyendo za baadhi ya viongozi wa dini wanaod aiwa kuchochea
mgawanyiko kwenye jamii.
SektayaU chumi
Alisema juhudi kubwa
zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha ukusanyaji wa mapato,uwezeshaji
na ush irikishaji wananchi katika harakati za kujenga uchumi.
Aliongeza
kuwa,ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka ambapo mwaka2010/2011
walikusanya sh. bilioni 181.4, mwaka 2011/2012 sh. bilion I 212 na mwaka
2012/13 ukusanyaji ulikuwa sh. Bilioni 266.2.
“Uchumi wetu unakua
kila mwaka, ulikuwa kwa asilimia 6.4 mwaka 2010, mwaka 2011 ulifikia
asilimi a 6.7 na 2012 ulikua kwa asilimia 7.0,mwaka huu utafikia
asilimia 7.5,” alisema.
Sektaya Miundombinu
Aliongeza kuwa,
Serikali yake imeweza kutekeleza vyema Ilani ya CCM ya mwaka 2010/2015,
Dira 2020 na MKUZAII katika sekta ya miun dombinu kwa kujenga barabara
mpya ambazo waliziahidi na nyingine kuzikarabati.
Sekta ya Elimu
Dkt.Shein
alisemani dhahiri kuwa maendeleo katika nchi yoyote yanategemea fursa
na elimu bora wanay oipata wananchi wake hivyo Serikali yake imeimarisha
sekta ya elimu kwa maendeleo ya nchi,kuongeza idadi ya shule na
walimu.
Sektaya Afya
Alisema ujenzi wa vituo 134 vya afya,
vimepunguza tatizo la wananchi kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma
ambazo hivi sasa zimeimarika.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment