Baadhi
ya watuhumiwa 10 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar
(JUMIKI) wakiwa katika moja ya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika
ajali ya Mali ya Mv. Skagit iliyotokea mwaka juzi 2012 na kuuwa watu
kadhaa.
ZANZIBAR: Mahkama Kuu Vuga Mjini Zanzibar imetoa dhamana na masharti
magumu kwa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu
Zanzibar (JUMIKI) ambao walisekwa rumande kwa zaidi ya mwaka sasa.
Akisoma hukumu Jaji wa Mahakama hiyo Fatma Hamid
Mahmoud aliwataka kila mshitakiwa kutoa fedha taslim milioni 25 kuwa na
wadhamini watatu ambao mmoja wao awe ni mfanyakazi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na awe na mali isiyo hamishika yenye thamani hiyo
hiyo ya milioni 25, na barua ya kiongozi wa mtaa (Sheha).
Hata hivyo licha ya dhamana hiyo uwzekano wa
washitakiw ahao ambao wanatakiwa kurudi mahamani 25 mwezi ujao
utekelezaji wa dhamana hizo umekuwa ni mgumu na wamerudishwa rumande
huku jamaa zao wakihanngaika kutimiza masharti hayo. Huyu hapa Wakili wa
watuhumiwa hao Abdallah Juma anasema.
Masharti mengine ni kuwa na kitambulisho cha
Mzanzibari Mkaazi, kuwasilisha hati ya kusafiria (Passport) Mahakamani
na kutoruhusiwa kusafiri hata kuvuka katika kisiwa cha Unguja bila ya
ruhusa ya Mahakama pamoja na washitakiwa hao kutoruhusiwa kuzungumza na
waumini wao kwa njia ya mihadhara ya nje wala misikitini isipokuwa
ruhusa ni kusaidilisha isiwe zaidi ya hapo.
Kutofanya wala kusababisha vitendo vyovyote venye kuashiria fujo kinyume na hilo watarudi rumande hadi kesi itakapokwisha.
Mapema mwendesha mashitaka wa serikali Rashid Abdallah aliwasilisha
pingamizi mbele jaji huyo za kuzuwia amri ya kuwataka kuwasilisha
sababu za kuzuwia dhamana za watuhumiwa hao.
Watuhumiwa hao ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni,Mselem Ali
Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa
Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa
Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar
Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa
Mwanakwerekwe , Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini na Majaliwa
Fikirini Majaliwa
Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu
mali, Uchochezi,Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula
njama ya kufanya kosa.
Kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan
Khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi
vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani ambapo Azzan hakuwepo
Mahakamani hapo kitendo kilichomfanya jaji Fatma kuhoji ni kweli
mtuhumiwa huyo anaumwa au ni unjanja wa kukosa kwenda mahakamani
“Mbona watuhumiwa hawa ni 9 mmoja yupo wapi hivi ni
kweli anaumwa hebu jamaa yake njoo hapa uninongoneze” alisema Jaji Fatma
ambapo anayemuwakilish Azzan alisogea na kuongea naye.
Kesi hiyo iliakhirishwa hadi Februai 27 mwaka huu na watuhumiwa
walirudi rumande hadi watakapokamilisha masharti ya dhamana zao huku
jamaa za watuhumiwa hao wakionekana kukimbilia majumbani na kuhangaikia
kupatikana kwa fedha hizo.
Akizungumza nje ya Mahakama hiyo Wakili wa upande wa Watuhumiwa Abdallah
Juma alisema masharti waliopewa wateja wake ni magumu mno na hivyo
hadhani kama wanaweza kuyatekeleza katika kipindi walichopewa.
“Masharti yaliotolewa ni magumu kutekelezeka na
kisheria masharti hayatakiwi yawe magumu kiasi kama hicho kwa kuwa
dhamana ni haki ya kila mmoja wetu na hivyo kupewa masharti magumu kiasi
hicho haipendezi lakini kwa kuwa Mahakama imeshaamua basi tutafata
utaratibu na tutarudi tena Mahakamani kuiomba mahakama ipunguze masharti
hayo” aliongeza Wakili huyo.
Wakili huyo amesema madhumuni ya kupewa dhamana sio
kumkomoa bali ni kumfanya mshitakiwa aweze kufika mahakamani hivyo bado
wao kama mawakili wana matumaini ya kurudi tena mahakamani na
kuishawishi mahakama iweze kupunguza masharti hayo ambayo ni magumu.
Chanzo;Zanzibar yetu
0 comments:
Post a Comment