Ndoto za karafuu kubinafsishwa Zanzibar imetoweka baada ya
Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui kuwasilisha
muswada wa sheria unaoipa nguvu Serikali kudhibiti zao hilo.
Pia, unaweka adhabu kali kwa mtu yeyote
atakayepatikana na hatia ya kuhujumu zao la karafuu au miti yake. Mswada
huo unafuata Sheria ya Karafuu Namba 11 ya mwaka 1985 na kuweka sheria
mpya ya maendeleo ya karafuu, ikiwamo kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo
ya zao hilo visiwani Zanzibar na kuweka masharti ya ukaushauji na kupiga
marafuku kuanikwa juu ya paa za nyumba.
Waziri Mazrui alisema kutakuwa na kikosi kazi
kitakachoteuliwa na kuongozwa na waziri, kifanya kazi zinahusiana na
uzalishaji, uuzaji na uendelezaji karafuu na kazi nyingine kitakazopewa
na waziri au bodi.
Alisema kifungu cha 13(1) kinakataza kwa mtu
yeyote kufanya vitendo vya kuchoma miti ya karafuu, kutengeneza mkaa,
kuangusha, kung’oa mkarafuu, kuchimba mchanga au udongo kwenye shamba la
mikarafuu au kufanya shughuli nyingine yoyote inayokatazwa na kanuni
kwa maendeleo ya zao hilo.
Pia, Waziri Mazrui alisema ni marufuku kutumia
mkarafu kwa ujenzi wa aina yoyote iwe mbao. kuchonga vinyago au mapambo
na atakayetaka kukata mkarafuu kwa madhumuni ya maendeleo ataomba kibali
kwa waziri.
Hata hivyo, Waziri Mazrui alisema mtu yeyote
atakayekwenda kinyume na sheria hiyo akipatikana na hatia, atalipa faini
si chini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka mitano au adhabu zote kwa
pamoja kulingana na uzito wa kosa.
Pia, sheria hiyo imempa uwezo waziri kutangaza
katika Gazeti la Serikali ndani ya Zanzibar kuwa, ni eneo la upandaji
karafuu na mtu yeyote atakusudia kuhamisha karafuu kavu au mbichi au
makonyo ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine lazima awe na kibali cha
sheha.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment