Home » » Bandari mpya kuchukua maelfu ya makontena

Bandari mpya kuchukua maelfu ya makontena

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema bandari mpya, itakayojengwa katika eneo la Kwampigaduri, itakuwa na uwezo wa kuchukua makontena 250,000 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Rashid Seif Suleiman alisema hayo katika hafla ya utiaji wa saini kuanza kwa ujenzi wa bandari hiyo mjini hapa mwishoni mwa wiki.
Alisema ufinyu wa nafasi ya Bandari ya Malindi, kwa kiasi kikubwa umelikosesha Shirika la Bandari mapato yake, ambayo ni tegemeo kwa Serikali ambayo kwa sasa inachukua jumla ya makontena 65,000 tu.
“Bandari mpya ya Kwampigaduri itakuwa ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua na kuhifadhi jumla ya makontena laki mbili na nusu kwa wakati mmoja, ambapo sasa uwezo wake ni kuchukua makontena 65,000,” alisema.
Akifafanua, alisema Bandari ya Malindi kwa sasa imezidiwa na wingi wa makontena, ambapo utendaji wa kazi umedorora kwa kiasi kikubwa na kulikosesha shirika hilo mapato.
Alisema shirika hilo limelazimika kuyahifadhi makontena mengi katika eneo la Hoteli ya Bwawani kwa muda, hatua ambayo imezusha malalamiko kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo watu wa mazingira.
Ujenzi wa bandari mpya ya Mpigaduri ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China. Ujenzi wake utaanza rasmi baada ya kazi za utiaji saini, itakayofanywa na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano.
Chanzo;Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...

Ama kweli mamlaka kamili ndani na nje ya nchi! Kwanini asitie saini waziri wa fedha wa Zanzibar?

Anonymous said...

Aibu ht kusema mbele za watu yani mpk atok mtu bara

Post a Comment

 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa