Home » » Vyama visiingize itikadi zao Bunge la Katiba- Faki

Vyama visiingize itikadi zao Bunge la Katiba- Faki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Bunge la Katiba
 
Naibu  Katibu Mkuu wa Chama cha UDP  Zanzibar, Juma Khamis Faki, amevitaka  vyama vya siasa kutoingiza itikadi za kichama kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa wajumbe wote wapo kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wanapata katiba bora itakayotoa haki kwa wote.
Kadhalika, wajumbe wengine  wawakilishi wa makundi mbalimbali wametakiwa kuacha kunyoosheana vidole kwa kuwa wanaweza kusababisha kupata katiba isiyokidhi matakwa  ya  taifa.

Mjumbe huyu wa Bunge Maalum la Katiba alisema hayo katika mahojiano na NIPASHE kufuatia na tabia ya baadhi ya wajumbe kutetea vyama na asasi zao.

Alisema: “Tupo kwenye bunge hili kwa ajili ya kuwakilisha Watanzania siyo kwa  kuendeleza itikadi ya chama kinachotetea masilahi yake,” alisema.

Mjumbe  huyo alisema washiriki wa wananchi wanatakiwa kuingia katika bunge kama taifa moja la Tanzania ili wapate  Katiba bora.

Alisema Watanzania  wanatarajia kupata katiba hiyo ambayo itatetea na kusimamia kila kundi katika jamii kuanzia ulinzi wa  haki za binadamu, urai, uvuvi na  kilimo bila ubaguzi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa