Home » » Katiba ya Zanzibar kurekebishwa

Katiba ya Zanzibar kurekebishwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu, amesema Katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho ili iende sawa na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Suluhu alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari, muda mfupi baada ya kuzungumzia mafanikio na changamoto za Muungano katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, mjini hapa jana.

Alisema marekebisho kwa Katiba ya Zanzibar yatafanyika baada ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumalizika.

“Tukimaliza marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania marekebisho ya katiba nyingine lazima yatafanyika ili kuwekana sawa tunakwendaje katika zetu,” alisema Waziri Suluhu.

Katiba ya Zanzibar imekuwa ikilalamikiwa kuwa inapingana na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, kuitambua Zanzibar kuwa ni nchi. 

Awali, alisema katika miaka 50 ya Muungano kumekuwa na mafanikio mbalimbali, ikiwamo amani na utulivu, kukua kwa demokrasia, kuwekwa haki za binadamu kwenye katiba na fursa ya kupata haki katika mahakama.

Aliyataja mafanikio mengine kuwa ni sekta ya kisiasa kuzidisha mshikamano na maelewano miongoni mwa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema mbali na mafanikio, pia kumekuwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo uelewa duni wa Watanzania kuhusu Muungano, vikwazo vya kisheria na ukosefu wa rasilimali fedha, ambao umekuwa ukisababisha maamuzi mengi yanayofikiwa kuchelewa kutekelezwa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa