Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANACHAMA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, wametakiwa kuacha tabia ya
kuwataja watu wenye asili ya Pemba pekee kuwa ndio wenye msimamo wa
kudai Serikali tatu, bali mfumo huo umependekezwa na watu wenye asili
tofauti.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chipukizi wa CCM, Bw.
Muhija Ali Kombo, katika kongamano la wana CCM lililofanyika mwishoni
mwa wiki iliyopita, Mtoni Wilaya ya Magharibi Unguja.
Alisema imekuwa kawaida kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwaandama watu
wenye
asili ya Pemba na kudai wao ndio wanaotaka Serikali tatu ambapo baadhi
ya watu kutoka Chaani, Makunduchi na Kitope wanashabikia mfumo huo.
“Mimi mwenyewe ni Mpemba lakini sishabikii mfumo wa Serikali mbili sasa unaposimama na kumtaja Mpemba kuwa ndo anayeshabikia
Serikali tatu unafanya kosa,” alisema.
Katika kongamano hilo, Bw. Muhija aliwataja baadhi ya viongozi ambao wana asili ya Unguja
lakini wapo CCM pia ni waumini wakubwa wa Serikali mbili.
Aliwataja
viongozi hao kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Bw. Hamza
Hassan Juma, Jimbo la Kitope Bw. Mbarouk Makame Mshimba na Jaku Hashim
Ayuob ambaye ni mwakilishi wa
Jimbo la Muyuni.
“Nimelazimika kuwataja kwa majina kwa sababu ya uchungu nilionao, kila mmoja wetu
anaposimama
anatajwa Mpemba lakini mimi, Mwnyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Bw.
Yussuf Mohammed na Bw. Baraka Shamte ni wapemba lakini mbona
hatushabikii mfumo wa Serikali tatu,” alisema.
Katika kongamano hilo, wanachama hao walitoa azimio la kuwataka wabunge na wawakilishi
wa CCM kusimama imara na kutetea mfumo wa Serikali mbili vinginevyo watakaporudi watafute
majimbo mengine ya kugombea 2015.
Kongamano hilo liliandaliwa na CCM likiwa na lengo la kutoa maazimio yao juu ya muundo wa
Muungano likitarajiwa kuendelea katika Mkoa wa Kaskazini Machi 29 mwaka huu.
chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment