Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kutoka Makao
Makuu Dar es Salaam Stella Vuzo akitoa ujumbe wa siku ya Kimataifa ya
kumbukumbu ya wahanga wa Utumwa na Biashara ya Utumwa ng’ambo ya Bahari
ya Atlantiki kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern
(hawapo pichani) walipotembelea maeneo yaliyokuwa yakiendesha Biashara
ya Utumwa Zanzibar.
Biashara
hiyo ya Watumwa ilifanyika kwa miaka 400 na kuhusisha zaidi ya Waafrika
milioni 15 na watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa waathirika wa
ukatili wa Utumwa na kuendelea kuteseka na madhara yaa biashara ya
Utumwa.
Bi.
Vuzzo alisema lengo la ziara hiyo ni kutaka Wanafunzi kujifunza madhara
ya biashara ya Utumwa jinsi ilivyofanyika na madhara yake na ili waweze
kusaidia katika jitihada za kuitokomeza biashara hiyo ambayo mpaka sasa
bado inaendelea kufanyika kimya kimya katika maeneo mbalimbali nchini
na kuwataka kuzijua haki zao za kibinadamu na kutogeuzwa bidhaa za
kuuzwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa udanganyifu wa kupelekwa
kufanya kazi nchini za kigeni.
Mtembezaji
wageni Peter Mashauri wa Kanisa la Mkunazini akiwapa maelezo wanafunzi
wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern ya Dar es salaam walipotembelea
maeneo ya Kihistoria yaliyokuwa yakiendesha Biashara ya Utumwa Zanzibar
katika siku ya Kimatafa ya kumbukumbu hiyo inayoadhimishwa kila mwaka
ifikapo Machi, 25
Wanafunzi
wa Sekondari ya Ubungo wakimsikiliza mtembezaji wageni (hayupo pichani)
wakiwa katika chumba kidogo kilichokuwa kikihifadhiwa watumwa waliokuwa
wakisubiri kusafirishwa kwa ajili ya kupigwa mnada katika Kanisa Kuu la
Mkunazini.
Wanafunzi
wa Ubungo Modern wakiangalia vitabu vya Historia ya Zanzibar
walipotembelea Kasri ya Wananchi Forodhani Mjini Zanzibar.
Wanafunzi wa Ubungo wakiangalia sehemu waliyokuwa wakihifadhiwa watumwa katika maeneo ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanafunzi
wakiangalia Bandari ndogo iliyokuwa ikitumika kupokelea na kusafirisha
watumwa katika maeneo ya Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja.
(PICHA NA
MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.)
0 comments:
Post a Comment