Home » » MABALOZI WA EU WAPONGEZA MATUMIZI YA FEDHA PEMBA

MABALOZI WA EU WAPONGEZA MATUMIZI YA FEDHA PEMBA

Mabalozi  wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) wamepongeza matumizi ya fedha zinazotolewa na Jumuiya hiyo katika kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo Kisiwani Pemba . 



Wamesema kuwa kutokana na matumizi mazuri ya fedha hizo , Jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi katika kuwasogezea wnmanchi wake huduma muhimu za kijamii ikiwemo skuli , maji na mawasiliano .



Wakizungumza katika ziara ya kutembelea miradi inayoendeshwa na Jumuiya  ya misitu ya Jamii Pemba , na kufadhiliwa na jumuiya ya nchi za Ulaya EU wamesema kuwa  wameridhishwa na mafanikio yaliyofikiwa na Jumuiya ya Misitu ya jamii Pemba .



Ujumbe huo wa mabalozi  kumi na moja wa  EU hapa nchini umesema juhudi zilizochukuliwa na jumuiya ya misitu ya jamii ya kujenga skuli katika kisiwa cha Kokota pamoja na kujenga tangi la kuhifadhia maji ya mvua ni moja ya mafanikio yaliyofikiwa na wataendelea kusaidia ili kuona mafanikio zaidi yanapatikana .



Kiongozi wa Ujumbe huo  Filiberto  Sebregondi  amesema kuwa EU itaendeleza juhudi zake kwa kusaidia jamii ya Zanzibar kuweza kufikia maendeleo ya kweli .



Naye Mkurugenzi wa Jumuiya ya Misitu ya Jamii Pemba Mbarouk Mussa  amesema kuwa EU imekuwa akisaidia katika miradi mbali mbali ya kijamii   ambayo inaibuliwa na wananchi .
Jumuiya ya misitu ya jamii pemba imepata ufadhili kutoka EU wa utoaji wa elimu kwa jamii juu ya kubaliana na mabadiliko ya tabia nchi na umefanyika katika shehia tano za Pemba ambazo ni Mtaambwe Kaskazini , Pujini , Uwandani , Vitongaji pamoja na Fundo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa