Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Zaidi ya wanafunzi 200
kati ya 363 wa shule ya Sekondari ya Msuka Wilaya ya Micheweni Pemba hawahudhurii masomo siku ya Ijumaa ya kila Wiki bila ya sababu za
msingi .
Waalimu wa shule hiyo wameyabainisha hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Kaskazini Pemba Mhe Dadi Faki Dadi alipofanya ziara aya kuteembelea katika
Shule hiyo .
Wamesema kuwa wanafunzi
hao wamekuwa na kawaida ya kujipa mapumziko siku ya Ijumaa hali ambayo
inachangia matokeo mabaya ya mitihani yao ya Taifa ambapo wameiomba Serikali ya Mkoa kusaidia
kupatikana kwa ufumbuzi wa kitendo hicho .
Akizungumza na walimu , wanafunzi pamoja na wajumbe wa
kamati ya shule hiyo , Mkuu wa Mkoa ameiagiza Wizara ya Elimu Wilaya ya
Micheweni kuchukua hatua za kinidhamu dhihdi ya wanafunzi ambao wameifanya siku ya Ijumaa kuwa ni
mapumziko yao .
Amesema kuwa Serikali
haiwezi kuona sheria , kanuni na taratibu zinavunjwa hivyo ni lazima suala hilo
likomeshwe mara moja ili kuejnga maadili mema kwa wanafunzi .
Afisa Elimu na Mafunzio
ya Amali Wilaya ya Micheweni Mbwana Shaame Said amesema kuwa wamepanga kukutana
na wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili kutafuta njia ya
kukabiliana na tatizo hilo .
0 comments:
Post a Comment