Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bila umoja na Tanzania Bara, Wazanzibari wataishia kuwa
“wakimbizi” kwani dalili zaonyesha visiwa vyao vitamezwa na Bahari ya
Hindi.
Hiyo ndiyo hoja mpya kuhusu mustakabali wa Muungano, iliyoibuliwa leo katika Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini hapa.
Dokezo hilo limetolewa na aliyekuwa Waziri wa
Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Terezya Huvisa katika
kikao cha baraza hilo Alhamisi asubuhi.
Mjumbe huyo anadai kuwa viashiria vyaonyesha
Unguja na Pemba zaweza kutoweka siku za usoni, hali itakayopelekea
wakazi wake kuwa Wakimbizi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
“Bila Muungano Zanzibar itakuwa na wakimbizi wa [sic] Climate Change,” amesisitiza Dk. Huvisa.
Suala jingine lilogusiwa Bungeni hapa leo ni
umiliki ardhi, huku mjumbe mmoja akidai kuwa kama haki ardhi
isipolindwa, atapiga kampeni vijijini ili Rasimu ya Pili ya Katiba
isipite.
“Kule kijijini tunapotoka sisi…ukifika tu ukauliza
suala la Katiba, utakachoambiwa ni migogoro ya ardhi, maeneo ya malisho
[na] miundombinu,” amesema Mabagda Mwataghu anayewakilisha Vyama vya
Wafugaji.
Bunge hilo pia lilikumbwa na sintofahamu ya muda
mfupi mara baada ya mwakilishi wa Taasisi za Elimu toka Zanzibar, Zeyana
M. Haji, kuangua kilio baada ya kupata taarifa za ghafla kuwa baba yake
amefariki.
Hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa baraza hilo,
Samuel Sitta, asitishe mdahalo kwa muda ili kutoa nafasi kwa mjumbe huyo
kusindikizwa nje ya ukumbi wa Bunge Maalum.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment