Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Sauda Mtondoo.PICHA|MAKTABA
Wilaya ya Mafia imetangaza mkakati wa kuwasaka kwa siri watu
wanaohusika na kuwapa mimba wanafunzi ili kuwachukulia hatua za
kisheria.
Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa
habari hizi, Mkuu wa Wilaya hiyo, Sauda Mtondoo alisema kuwa hatua hiyo
inalenga kutetea haki ya watoto wa kike wanaokatishwa masomo kutokana na
ujauzito.
“Tatizo la kukatiza masomo kwa mimba lipo hapa
Mafia, lakini nimeanzisha mikakati wa kuhakikisha linatokomezwa. Kwa
kushirikiana na Shirika la Action Aid, Polisi na walimu tunaendesha
mkakati huo wa siri,” alisema Mtondoo.
Alifafanua kuwa hatua hiyo inatokana na wazazi na
walezi wengi wa watoto wa kike wilayani humo kushindwa kutoa ushahidi wa
matukio ya watoto wa kike kupewa ujauzito sababu kubwa ikiwa uhusiano
wa kidugu baina ya aliyepewa ujauzito na mvulana.
“Utakuta aliyempa binti ujauzito ni binamu yake,
hapo wazazi huamua kukaa kimya kwani wakitoa ushahidi wanaogopa hatua za
kisheria zitaathiri familia,”alisema.
Alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kesi
zisizopungua nne za watoto wa kike kupewa ujauzito hufikishwa mahakamani
kila mwaka, lakini ushahidi hukwama.
“Sasa walimu wamekubali watawasiliana kwa siri
nami moja kwa moja ili hatua zifuate mkondo kwa siri na katika hilo sina
msalie Mtume,” alisema Mtondoo
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment