Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Sheikh
Mkuu wa Msikiti wa Asili wa Ijumaa Micheweni Mjini Sheikh Haji Khatib
Haji.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara maalum
ya kuwakagua baadhi ya wazee katika sehemu mbali mbali ya Kisiwa cha
Pemba ili kujua haliu zao pamoja na kuwapa mkono wa pongezi kwa
kukamilisha mwaka 2014 na kuwatakia kheri ya mwaka mpya wa 2015.
Balozi
Seif akitoa Mkono wa Pole kwa Watoto na Wajukuu wa Muasisi wa Afro
Shirazy Party Marehemu Bibi Ashura Abeid hapo Nyumbani kwa Tibirinzi
Chake chake Pemba.
Balozi
Seif akibadilishana mawazo na Mzee Khamis Mkadara Khamis wakati
alipokwenda kumkagua na kumtakia kheir ya Mwaka Mpya wa 2015.
Mzee
Bakari Khamis Kombo wa Kijiji cha Micheweni akisalimiana na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kumjulia hali na
kumtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015.
Balozi
Seif akimsalimia mzee Khamis Othman Kapona wa Kijiji cha Chekea
Mtambwe alipokwenda kumtembelea na kujua hali yake pamoja na kumpa kheri
ya mwaka mpya.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtakia kheri ya
mwaka mpya wa 2015 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jimbo la Micheweni Mzee
Kombo Fundi Kombo wakati alipomtembelea na kujua hali yake.(Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment