Home » » SEIF ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR

SEIF ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha mkoba wenye Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akimkabidhi  Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisoma taarifa ya muongozo kwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Maalim Seif alisindikizwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine wanaounda UKAWA.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Kulia kwake ni Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa