Ismail Jussa akikanusha taarifa za uvumi kuhusu Maalim Seif.
Kaimu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ismail
Jussa amekanusha uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu
taarifa za kufariki dunia kwa makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif
Sharif Hamad na kusema wanaofanya hivyo ni watu wenye nia ovu na
kiongozi huyo.
Awali kabla
Jussa hajatoa taarifa hizo, Kituo cha ITV kilikanusha taarifa hizo za
upotoshwaji kupitia mitandao ya kijamii ambazo zilikihusisha, na
kuwaomba wananchi kuzipuuza maana si za kweli.
Kupitia ukurasa wao wa Facebook, ITV waliandika hivi: Kumekuwepo
wa taarifa za upotoshwaji kupitia mitandao ya kijamii na kuihusisha
ITV, tunaomba taarifa hizo zipuuzwe kwa kuwa taarifa hizo si kweli.
Taarifa zetu zinakuwa na vyanzo vya kuaminika, ITV haihusiki kwa namna
yeyote na taarifa hii. Tunaomba Watanzania wawe makini na Mitandao feki
inayozusha matukio na kutoa taarifa zisizo za kweli. Tunaomba vyombo
husika kuendelea kuwafuatilia na kuwabaini na kuwaweka hadharani watu
kama hawa.
Sehemu ya taarifa hiyo ya upotoshaji.
Chanzo GPL
0 comments:
Post a Comment