Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki dua ya kuuombea
Mwili wa Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati alipofika nyumbani kwa
marehemu fuoni michezani Unguja kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia leo
asubuhi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Mjane wa Marehemu
Ramadhani Nyonje Panda alipofika nyumbani kwao fuoni michezani kutowa
mkono wa pole kwa wana familia, kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh
Khamis Haji Khamis.
WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wac Jimbo la Muyuni Zanzibar.
WANANCHI wakiwa katika msiba wa
marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakiwa nyumbani kwa marehemu fuoni
michezani Unguja wakisubiri taratibu za mazishi ya marehemu kupelekwa
kijiji kwao Paje kwa mazishi.
WANANCHI wakisoma hitma ya marehe katika msiki wa fuoni kabla ya kusaliwa kwa ajili ya mazishi kijijini kwao Paje leo asubuhi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi katika
kisomo cha hitma ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu, iliosomwa katika
msikiti wa fuoni.
WANANCHI wakiitikia dua baada ya kusomwa kwa hitma ya marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati ikisomwa na Shekh Soraga.
WANANCHI wakiwa na jeneza likiwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu kwa ajili ya kusaliwa katika msikiti wa fuoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kubeba
jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi
kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi na Wananchi
wakishiriki katika Sala ya kumsalia marehemu Ramadhani Nyonje Pandu
iliofanyika katika msikiti wa fuoni na kuzikwa kijijini kwao Paje Wilaya
ya Kusini Unguja.
(Picha na Ikulu)
0 comments:
Post a Comment