Home » » Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni Atembelea Miradi ya Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni Atembelea Miradi ya Jimbo lake.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Yussuf Masauni na Aliyekuwa Mwakilishi wa Rahaleo kwa sasa ni Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jazira wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mbunge Mhe Masauni kutembelea Mradi wa Maji kaburikikombe Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akiwa katika ziara yake kutembelea mradi wa kisima cha maji kaburukikombe migimbani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Tanzania Youth Icon Abdalla Ahmeid akizungumza kuhusiara na mradi mkubwa wa Kisima cha Maji kilichofadhiliwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakati wa ziara ya Mhe Mbunge Hamad Masauni katika jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa ziara yake katika mradi wa maji kaburi kikombe migombani Zanzibar Mradi huo unasimamiwa na Jumuiya ya TAYI  Tanzania Youth Icon kulia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo na kwa sasa anagombea Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salim Jazira. 
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani akimsikiliza Mhe Mbenge wakati wa ziara yake katika kisima cha maji kaburi kikombe migombani Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni akiangalia mradi wa kisima kipya kinachosimamiwa na TAYI kinachochimbwa katika eneo la Kaburi Kikombe Zanzibarb hicho kitakuwa kisima cha Pili kuchimbwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kikiwa na urefu wa mita 42 kinachotarajiwa kukamilika kwake kutumia shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwake.
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni akiangalia mradi wa kisima kipya kinachosimamiwa na TAYI kinachochimbwa katika eneo la Kaburi Kikombe Zanzibarb hicho kitakuwa kisima cha Pili kuchimbwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kikiwa na urefu wa mita 42 kinachotarajiwa kukamilika kwake kutumia shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwake.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya TAYI Abdalla Ahmeid akitowa maelezo ya mradi huo wa Pili wa Uchimbaji wa Kisima cha Maji kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na jirani zake kikiwa katika hatu ya mwisho ya uchimbaji wake. 
Katibu Mtendaji wa TAYI Abdalla Ahmeid akitowa maelezo ya uchimbaji wa kisima hicho kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mhe Mbunge Hamad Masauni.
Afisa Rasilimali Maji wa Mamlaka ta Maji Zanzibar ZAWA Hassan Zaharan Said, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kisima cha maji, wakati wa ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar. 
Afisa Rasilimali Maji wa Mamlaka ta Maji Zanzibar ZAWA Hassan Zaharan Said, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kisima cha maji, wakati wa ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar



Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni na Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Mbunge wa Kikwajuni Zanzibar uliofanyika katika Kituo cha Jumuiya ya TAYI muembemadema Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani wakimsikiliza mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni ambaye alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa mkutano huo wa maadhimisho ya ziara ya Mbunge wa Kikwajuni. 
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Masauni katika ukumbi wa Jumuiya ya TAYI muembemadema Zanzibar wakati wa kakamilisha ziara ya Mbunge wa Kikwajuni Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake katika ukumbi wa Chuo cha TAYI muembemadema baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja kutembelea miradi ya Jimbo la Kikwajuni Zanzibar. 
Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikilia Mbunge wao wakati wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maji na Kituo cha Vijana cha Tanzania Youth Icon muembemadema kinachotowa elimu ya Ujasiriamali kwa Vijana mbalimbali wa Jimbo la Kikwajuni na jirani zao. 
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akizungumza nao baada ya ziara yake katika jimbo hilo.
Vijana wa Jimbo la jangombe wa uhamasishaji wakiwa katika ukumbi wa TAYI Miembeni wakimsikiliza Mhe, Masauni.akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake baada ya ziara yake kutembelea Miradi ilioko katika Jimbo hlake inayosimamiwa na TAYI.
Mgombea Udiwani wa Wadi ya Miembeni Mbarouk Abdalla Hanga akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni baada ya kumaliza ziara yake kutembelea miradi ya Maji ya Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wakisoma dua baada ya kumaliza ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Eng.Hamad Yussuf Msauni wakiwa katika Kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.


0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa