Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi
(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameithibitishia rasmi Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (Zec) kujiondoa kuwania wadhifa huo katika Uchaguzi wa marudio
utakaofanyika Machi 20, mwaka huu.
Mbali na Maalim Seif, wagombea wote wa chama hicho wa nafasi ya
Uwakilishi na Udiwani wamejiondoa kwa kuwasilisha barua rasmi kuwa
hawatoshiriki uchaguzi huo wa marudio wa Zanzibar.
Akizungumza na Nipashe Mjini Zanzibar, Mkurugenzi wa Mipango na
Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema Maalim Seif amewasilisha waraka
wa barua wa kujiondoa kwa Zec, Febuari 8, mwaka huu.
Alisema hatua aliyochukuwa mgombea huyo ni utekelezaji wa wa azimio
la Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kutoshiriki uchaguzi mkuu wa
marudio visiwani hapa.
Shehe alisema kuwa Zec imetakiwa kutotumia jina wala picha za
Maalim Seif taarifa zozote katika karatasi za wapigakura kabla ya
kufanyika uchaguzi huo.
Alisema kuwa katika Barua yake Maalim seif amesisitiza kuwa
uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana ulikuwa uchaguzi huru na wa haki na
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha salim Jecha hakuwa na
mamlaka ya Kikatiba na sheria kufuta matokeo ya Uchaguzi huo.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Kassim
alisema jana kuwa ni mapema kueleza vyama vingapi vimekamilisha
kuthibitisha wagombea wake kama wapo hai na watashiriki uchaguzi kabla
ya kufanyika Machi 20, mwaka huu.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment