Zubeir Ali Maulid
Hatimaye
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama Cha Mapinduzi
Zanzibar leo wamefanya Uchaguzi wa kumpata mjumbe atakaye peperusha
bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Spika wa Baraza hilo,
kwa kipindi cha mwaka 2015 – 2020.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
waIdara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu, amesema uchaguzi
huo ulioendeshwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi, ulifanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Unguja.
Mwenyekiti
wa Uchaguzi huo, uliojumuisha wajumbe 72, alimtangaza Zubeir Ali Maulid
(Pichani) kuwa mshindi baada ya kupata kura 55 na kuwashinda wapinzani
wake wawili aliyemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho aliyepata kura 11
na Jaji Janeth Nora Sekihola aliyepata 4, na kura mbili (2)
ziliharibika.
Jumla ya wanachama wa tisa (9) walijitokeza kuomba ridhaa ya CCM ili wagombee nafasi hiyo ya Spika .
Katika
kikao cha Kamati Maalum kilichofanyika Machi 24, mwaka huu, Afisi Kuu
ya CCM Zanzibar, ilipitisha majina matatu ikiwa ni pamoja na Pandu
Ameir, Zubeir Ali Maulid na Janeth Nora Sekihola, ambapo uchaguzi wake
umefanyika leo.
Akitoa
neno la shukrani, Zubeir Ali Maulid, aliwashukuru wajumbe hao kwa imani
yao kwake na kuwataka wampe kila aina ya mashirikiano ili aweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Naye
aliyekuwa Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho, amekubali kushindwa
na kumuahidi kumpa msaada wowote atakaohitaji, iwapo atatakiwa kufanya
hivyo.
Zubeir Ali Maulid
0 comments:
Post a Comment