Home » » SERIKALI KUJENGA NYUMBA 4139 ZA ASKARI POLISI KATIKA MIKOA 17 NCHINI.

SERIKALI KUJENGA NYUMBA 4139 ZA ASKARI POLISI KATIKA MIKOA 17 NCHINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



 
Na Ismail Ngayonga

MAELEZO


13.6.2016

SERIKALI katika mwaka 2016/17 imepanga kujenga nyumba 4139 za askari wa jeshi la Polisi nchini, hatua itakayosaidia kukabiliana na uchache wa nyumba za kuishi kwa askari hao.

Awamu ya kwanza ya nyumba hizo zinatarajiwa kujengwa katika mikoa 17 nchini ikihusisha mikoa ya Tanzania Bara pamoja na mikoa ya Unguja na Pemba.

Akijibu  swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Faida Mohammed Bakar, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema Serikali itaendelea kuboresha makazi ya askari na ofisi za polisi kwa awamu kwa kadri hali ya kiuchumi itavyoimarika.

Ole Nasha alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili askari polisi katika maeneo mbaliombali nchini ikiwemo uchakavu wa ofisi, ambapo kwa kuanzia imeamua kuanza mpango wa kukarabati ofisi na makazi ya askari wake.

Aidha alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa inatoa mikopo ya vyombo vya usafiri kwa askari wake ambao wanaishi mbali na vituo vyao vya kazi ili kuwasaidia kuwahi katika maeneo yao ya kazi kwa wakati.

“Serikali inatambua changamoto inayowakabili askari wetu nchini ikiwemo wale wa Kusini Pemba, katika kukabiliana na hali hiyo tumepanga sasa kuifanyaia ukarabati miundombinu ya ofisi hiyo sambamba na ujenzi wa makazi bora kwa askari wetu” alisema Ole Nasha.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kujenga nyumba za kuishi Na ofisi za kisasa katika kituo cha mkoani na kengeja Pemba.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa