Home » » BALOZI SEIF ALI IDDI AMJULIA HALI MWAKILISHI WA JIMBO LA UZINI MH. MOHAMED RAZA HASSANALI

BALOZI SEIF ALI IDDI AMJULIA HALI MWAKILISHI WA JIMBO LA UZINI MH. MOHAMED RAZA HASSANALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimjulia hali Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohamed Raza Hassanali hapo Hotelini Kwake Golden Tulip Kibweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Mh. Raza anaendelea na mapumziko mafupi baada ya kufanyiwa matibabu Nchini India hivi karibuni. Aliyepo nyuma yao ni Mdogo wake Mh. Mohamed Raza ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kimbesamaki Mh. Ibrahim Raza.
 Mh. Mohamed Raza kati kati akieleza namna alivyopata huduma za Afya wakati akiwa Hospitalini Nchini India. Wa kwanza kulia ni Balozi Seif na kulia ya Mheshimiwa Raza ni Daktari Azan anayefuatilia afya yake katika kipindi hichi cha mapumziko.
Dr. Azan akimueleza Balozi Seif baadhi ya njia anazopaswa Mtu kuzichukuwa  katika kujilinda dhidi ya maradhi ya Kisukari makubwa zaidi ni kufuata miko ya vyakula na kufanya mazoezi kila siku. 
Picha na OMPR – ZNZ.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa