Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Baraza
la Manispaa Wilaya ya Mjini linakusudia kutoa zawadi kwa shehiya za
Wilaya hiyo ziakazofanya vizuri zaidi katika uhifadhi na utunzaji
Mazingira.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Kituo cha afya Chumbuni Mkurugenzi wa
Baraza hilo Aboud Hassan Serenge alisema lengo la kutoa zawadi hizo ni
kuwashajiisha wanachi kujenga tabia ya kutunza mazingira ikiwa ni moja
ya njia ya kupambana na maradhi ya mripuko.
Alisema
Baraza la Manispaa litaendelea kushirikiana na viongozi wa Majimbo ya
Wilaya hiyo kwa kutoa Vifaa vya kufanyia usafi ili kuhakikisha
Mazingira ya mji yanakuwa salama kwa maisha ya wananchi .
“Sisi
kama Baraza la Manispaa nijukumu letu kuhakikisha Mazingira yanakuwa
masafi hivyo tutashirikiana kwa karibu na Majimbo kutowa Vifaa vya
usafi ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa katika hali ya usalama “Alisema
Mkurugenzi huyo.
Hata
hivyo alisema kuwa kwa wale ambao watajikusanya pamoja na kufanya
usajili unaokubalika watawatengenezea mazingira mazuri ya kuhakikisha
wanapata ada ya kazi wanayoifanya sambamba na ada ya Vifaa.
Vile
vile alieleza kuwa miongoni mwa vitu wanavyo zingatia katika Bajeti yao
ni kutoa vifaa kwa ajili ya usafi wa mazingira ili kuepusha kutokea kwa
maradhi ya Miripuko .
Sheha
wa Shehia ya Kwamtumwajeni, Jimbo la Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa
alisema suala la usafi wa mazingira amelipokea vizuri na kwa
kushirikiana na wananchi ameahidi watalisimamia kwa ukamilifu licha ya
chaangamoto ziliopo.
Alizitaja
Changamoto hizo kuwa ni pamoja na muitiko mdogo wa baadhi ya wananchi
juu ya suala hilo, ukosefu wa vifaa na kukosekana Sehemu ya kuwekea
taka (Madampo).
Sheha
Ngauchwa amewataka Wananchi wa Shehia yake kurejesha utamaduni wa
zamani wa kusafisha mazingira yaliyowazunguka kwa hiari bila ya
kushurutishwa jambo ambalo litasaidia kufanikisha kuweka Mazingira Safi.
“Ningependa
kuwasisitiza tushirikiane pamoja kuweza kuweka mazingira yetu kuwa safi
bila ya kutegemeana na kubaguwana kwa Siasa zetu kwani suala la usafi
halitaki siasa,”Alisema Ngauchwa.
Nao
Wananchi kutoka Shehia mbali mbali Jimbo la Magomeni Walisema kuwa
suala la kuweka Mazingira safi sio suala la kuwaachia Manispaa kufanya
usafi peke yao bali suala hilo linamuhusu kila mmoja wetu.
Sambamba
na hayo wamesema suala la kutunza mazingira ni suala muhimu na kila
mmoja anajukumu la kuhakikisha mazingira yaliyomzunguka yanakuwa
salama wakati wote.
0 comments:
Post a Comment