Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jamii
imetakiwa kujisomea sheria mbali mbali zinazohusu ardhi, ili kujiepusha
na migogoro, inayoweza kujitokeza wakati wanapotaka kuitumia kwa kazi
tofauti, ikiwa ni pamoja na ujenzi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC
Tawi la Pemba, Bi.Fatma Khamis Hemed alipokuwa akiwasilisha mada ya
sheria na matumizi ya ardhi no 12 ya mwaka 1992, kwa wasaidizi wapya wa
sheria, kwenye mafunzo yaliofanyika mjini Chakechake.
Alisema,
zipo sheria saba zinazohusu masuala ya ardhi ikiwemo ya sheria ya
kumtambua na kumthibitisha mwenye kumiliki ardhi no 8 ya mwaka 1990,
sheria ya mahakama ya ardhi no 7 ya mwaka 1994.
Alieleza
kuwa sheria nyengine ambazo jamii inapaswa kuzielewa, ni ile ya
kamisheni ya ardhi ya mwaka 2015 sambamba na sheria ya usajili wa ardhi
no 10 ya mwaka 1990, ambayo inaelezea umuhimu na ulazima wa kusajili
ardhi.
Hivyo
Mratibu huyo wa ZLSC, amesema kwa vile hakuna kinga kwa mtu asiyejua
sheria, ni vyema kwa jamii ikafanya juhudi za kuzielewa.
“Jamii
ikitumie kituo chetu kujifunza mambo mbali zikiwemo sheria za ardhi na
nyengine, ili wajiepushe na migogoro isiyokuwa ya lazima”,alieleza.
Kwa
upande wake, Hakimu wa Mahakama ya ardhi Pemba Mhe. Khamis Rashid
akiwasilisha sheria ya Mahakama hiyo no 7 ya mwaka 1994, alisema lengo
la kuwepo kwa mahakama hiyo, ni kupunguza mrundikano wa kesi, kwenye
mahakama za kawaida.
“Kabla
ya kuwepo kwa mahakama hii, ilikuwa kesi zote zinazohusiana na ardhi
zilikuwa kwenye mahakama nyengine, lakini kuanzia mwaka 1994, zimeanza
kusikilizwa na mahakimu maalum”,alifafanua.
Nae
Naibu Mrajisi wa usajili Asha Suleiman Said, alisema lengo la
kuanzishwa kwa kamisheni hiyo ni kuwa na chombo kimoja cha kusimamia
ardhi, ambapo hapo kabla kulikuwa na taasisi tofauti zilizokuwa na kazi
moja.
Aidha
alieleza kuwa, kazi nyengine ni kuweza kuifanyia tathmini ardhi na
kuanziasha kodi, hivyo ni wajibu wa jamii na wasaidizi wa sheria kuisoma
na kuielewa.
Wakichangia
mada kwenye mafunzi hayo, wasaidizi hao wa sheria walisema, elimu kwa
jamii inahitajika sana hasa kwa vile zipo sheria saba zinazozungumzia
masuala ya ardhi.
Msaidizi wa sheria kutoka Jimbo la Chambani Idrisa Khamis alisema sheria zipo nzuri, ingawa jamii imekuwa ikikosa kuzielewa.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yaliowashirikisha wasaidizi wa sheri kutoka majimbo
ya uchaguzi kisiwani Pemba, mada kadhaa zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na
usajili wa ardhi no ya mwaka 1990, sheria ya kamisheni ya ardhi ya
mwaka 2015 pamoja na sheria ya matumizi ya sheria ardhi no 12 ya mwaka
1992.
0 comments:
Post a Comment