Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa
Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya siku moja kwa
walinzi wanaolinda Hospitali za Serekali na kuwataka wawe wakarim katika
kutoa huduma.
Mkurugenzi
Utawala na Uendeshaji wa Hospitali ya Mnazimmoja Abubakar Khamis Hamadi
akitoa maelezo ya mafunzo yakuwajengea uwezo zaidi walinzi wanaolinda
Hospitali, mafunzo hayo yamefanyika Hospitali ya Mnazimmoja Mjini
Zanzibar.
Baadhi ya walinzi katika mafunzo wakifuatilia hutuba ya NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said hayupo pichani.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman katika picha ya pamoja na walinzi wanaolinda Hospitali za Serekali.(Picha na Makame Mshenga)
Na Maryam Kidiko - Maelezo Zanzibar.
NAIBU Waziri wa
Afya Harusi Said Suleiman amewataka Walinzi wa Hospitali ya Mnazi
Mmoja kubadilika katika utendaji wa kazi zao ili kuongeza mashirikiano
kati yao na wananchi wanaokwenda kwa ajili ya kupata huduma mbali
mbali katika hospitali hiyo
Hayo aliyasema
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwenye Mafunzo ya Siku moja ya Walinzi
wa Hospitali hiyo ambayo yanalengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi
zao na kuongeza Mashirikiano na wateja wao.
Aliwaeleza
walinzi hao kuwa kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya walinzi wamekuwa
wakitumia lugha mbaya kwa wagonjwa na wananchi wanaofika kuangalia
wagonjwa wao jambo ambalo sio zuri.
Aliwasisitiza
walinzi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutumia lugha nzuri kwa Wagojwa kwani
kufanya hivyo itapelekea kujenga mashirikiano katika utendaji mzima wa
kazi yao.
Alisema
kunatofauti kubwa kati ya ulinzi wa Hospitali na ulinzi katika sehemu
nyengine kwani mara nyingi wananchi wanaofika Hospitali wanahitaji
kuhurumiwa kutokana na mazingira wanayokuwa nayo.
“Walinzi wetu
tunawaamini sana na tunajuwa mnakumbana na changamoto nyingi lakini ni
lazima mtumie akili za ziada ili Wagojwa wanapofika wajiskie furaha
hatakama wapo katika huzuni,”Alisema Naibu Waziri.
Hata hivyo
alishauri zinapotokea Changamoto ndogo ndogo kuzishughulikia kwa njia
nzuri za ushirikiano kwa pande zote zinazohusika .
Aidha aliwaeleza
walinzi hao kuwa baada ya kupata mafunzo hayo Serikali haitawavumilia
kuona wanaenda kinyume na utaratibu uliowekwa katika kuwahudumia
wananchi.
Mkurugenzi
Utawala na Uendeshaji wa Hospitali ya Mnazimmoja Abubakar Khamis Hamadi
alisema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza mashirikiano mazuri kati ya
Wagojwa, wananchi wanaofika kwa ajili ya kuangalia wagonjwa na Walinzi.
Alieleza
matumaini yake kuwa mafunzo hayo yatawawezesha Walinzi kujuwa njia
sahihi za kuwashuhulikia wateja wao wanapofika katika Hospitali na
kujuwa wajibu wao.
“ Tunapata
malalamiko mengi kutoka kwa Wagojwa hivyo tumeamuwa kutowa mafunzo hayo
kwa Walinzi ili kuondoa matatizo na kuongeza mashirikiano mazuri baina
yao,” alisema Mkurugenzi huyo.
Aliwataka walinzi
waliopata mafunzo hayo kuyafanyia kazi ili kutimiza lengo la mafunzo
yenyewe na kuleta ufanisi katika kazi yao bila kutokea malalamiko
mengine.
Mkurugenzi
Abuubakar amewaomba Wananchi wanaofika hospitalini hapo kutowa
mashirikano mazuri kwa Walinzi na iwapo litatokezea tatizo wafike katika
kitengo cha huduma kwa Mteja kwa lengo la kushughulikiwa.
Msaidizi Mkuu wa
Walinzi Aboubakar Hassan Bakari aliahidi baada ya mafunzo hayo
watabadilika na kuwashauri walinzi wenzake kuwa waadilifu huku wakijua
wao ni kampuni ya ulinzi ya Kibiashara hivyo wanatakiwa kuvutia waajiri
wao.
0 comments:
Post a Comment