Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akikagua madarasa ya
skuli ya msingi Jang’ombe ‘B’ yaliyofanyiwa ukarabati na kampuni ya Bima
Jubilee ikiwa ni sherehe ya kutimiza miaka 80 tokea kuanzishwa. Kulia,
ni Mwalim Mkuu wa skuli hiyo Bi. Salila Adam Sadik.
Mkuu
wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa madarasa sita yaliyofanyiwa ukarabati na kampuni ya Jubilee
katika skuli ya Jang’ombe ‘B’. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa mamlaka
ya usimamizi wa Bima Zanzibar Mohammed Ameir, akifuatiwa na Meneja wa
Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman pamoja na Mwenyekiti wa kamati
ya skuli ya Jang’ombe ‘B’ Taifani Vuai Makame.
Mkuu
wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akimtunuku cheti Meneja
wa kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman kwa kuthamini
mchango wake wa kampeni ya mimi na wewe katika hafla iliyofanyika skuli
ya msingi Jang’ombe mjini Zanzibar.
Meneja
wa Kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman (katikati)
katika picha maalum na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed
Mahmoud pamoja na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Jang’ombe ‘B’ Bi. Salila Adam
Sadik. Picha na Makame Mshenga
Na Miza Kona-MAELEZO ZANZIBAR
Mkuu
wa Mkoa Mjini magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, ameitaka Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali kuweka mpango maalum wa kuyafanyia matengenezo
madarasa na madawati pale yanapoharika ili kuepusha hasara.
Ameyasema
hayo huko Skuli ya Msingi Jang’ombe katika hafla ya Uzinduzi wa
Madarasa sita yaliyofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Bima ya Jubilee
katika kusheherekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema
mpango huo mbadala utasaidia kupunguza gharama za matengenezo na kuweka
majengo katika mazingira mazuri yatayomwezesha mwanafunzi kusoma katika
hali ya kuridhisha.
Alisema
kuwepo utaratibu wa kuwatoza fidia kwa mwanafunzi au raia yeyote
atakaharibu kitu ili kuweza kudhibiti majengo na vifaa vya skuli na
kuiepushia serikali hasara ya kuyafanyia matengenezo kwa gharama kubwa.
Alieleza
kuwa serikali inachukua jitihada ili kuhakikisha skuli zote zake zote
zinapatiwa madawati ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
“Tatizo la madawati katika skuli litafikia ukomo wake mwishoni mwa mwaka huu,” alifahamisha Mhe. Ayoub.
Mkuu
huyo wa Mkoa amewaomba wazazi na walezi kujiunga na bima ya elimu kwa
ajili ya watoto wao ili kuwekeza katika elimu na kuwajengea mazingira
mazuri ya maisha yao ya baadae.
Aidha
alieleza kuwa kuna changamoto nyingi katika jamii hasa kwenye sekta ya
elimu na afya, hivyo jamii inatakiwa kushirikiana ili kuzipatia ufumbuzi
wa pamoja kasoro zinazojitokeza.
Ayoub
pia ameipongeza kampuni ya Bima ya Jubilee kwa mchango wake huo wa
kiunga mkono serikali katika sekta ya elimu na kuwataka wadau wengine
kutoa michango yao katika huduma za kijamii ili kuleta maendeleo nchini.
Alikabidhi
cheti kampuni hiyo kwa kuwa mdau mkuu wa kutoa mchango katika huduma za
jamii na kuunga mkono kampeni ya Mimi na Wewe.
Akisoma
risala, Meneja wa kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman
alisema kampuni yake imejitolea kukarabati madarasa sita katika sehemu
zilizobomoka, sakafu pamoja na kuta, kuweka madirisha, milango na kupaka
rangi ndani na nje ili kuwaondoshea watoto kero zinazowakabili na
kujali afya zao wakati wa masomo.
Aidha
ameitaka jamii kuzitunza mali za serikali kwa kuzingatia kwamba skuli
ni mali ya jamii hivyo ni wajibu kuzienzi na kuzilinda ili ziweze
kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Mapema
akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya skuli ya Jang’ombe
Taifani Vuai Makame, alisema tatizo kubwa la skuli hiyo ni kuvuja kwa
paa lake wakati wa mvua, hali inayofanya wanafunzi wasiweze kuendelea na
masomo.
0 comments:
Post a Comment