Home » » Mgogoro kati ya wavuvi wa Kojani, Kiungoni wamalizika

Mgogoro kati ya wavuvi wa Kojani, Kiungoni wamalizika

Mkuu wa Wilaya ya Wete Bw Omar Khamis Othman amewapongeza wavuvi wa Kojani na Kiungoni  kwa kukubali kumaliza mgogoro na kurejesha uhusiano na ushirikiano na kuwataka kuzika tofauti zote bali wawe tayari kushirikiana pamoja na katika kufanikisha masuala ya maendeleo .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema kuwa wavuvi hao wameuahidi kurejesha uhusiano wao pamoja na kuendeleza ulisimamizi ulinzi na udhibiti wa uvuvi haramu katika bahari ya shehia hizo.

Amesema kuwa mgogoro huo ulisababisha kuchuliana kwa vifaa vya uvuvi kwa kila upande ambapo wavuvi wa Kiungoni walizuia mitego ya wavuvi wa Kojani ambapo wakojani nao walizuia vyombo vya uvuvi za wavuvi pamoja na nyavui za wavuvi wa Kiungoni.

Nao wajumbe wa kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete kushughulikia mgogoro huo wamesema kuwa wavuvi wa Shehia hizo wamekubaliana kusameheana ili kulinda udugu na uhusiano wa enzi wa wananchi wa shehia hizo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Khamis Shaaban Hamad amefahamisha kwamba, kumalizika kwa mgogoro huo kutawafanya wananchi hao kuimarisha ushirikiano wao wa zamani ambao uliasisiwa na babu zao.

Aidha amesema kuwa pamoja na kwamba haikuwa rahisi kufanikisha makubaliano hayo, lakini anawashukuru wazee wa pande hizo kwa kuhakikisha kwamba amani ambayo ilikuwa imeanza kutoweka kurejea .

Kwa upande wao wavuvi kutoka kutoka Kiungoni amesema kuwa wao wamesamehe vifaa vyao ambavyo vimachukuliwa na kushindwa kurejeshwa na wavuvi wa Kojani baada ya kubaini kwamba mgogoro huo hauna mwisho mzuri.

Mgogoro huo ulitokea baada ya wavuvi wa Kiungoni kudai kwamba wavuvi kutoka Kisiwa cha Kojani kuendesha uvuvi haramu katika bahari ya Kiungoni ambayo inahifadhiwa jambo ambalo liliwafanya kuichukua mitego ya wakojani, ambapo wakojani nao waliivamia bandari ya Kiungoni na kuchukua vyombo vya uvuvi vya wavuvi wa Kiungoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa