Mwakilishi
wa Jimbo la Uzini Mohd Raza Hassan akitoa shukrani kwa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, baada ya kukabidhi Mashine ya Fotokopi Uongozi wa Skuli ya Msingi Uzini Ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Mwalimu Mkuu
Msaidizi wa Skuli ya Msingi Uzini Mwalimu Tatu Ame Suleiman akiambatana
pia na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohd Raza Hassan. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
*******************************************
Na Othman Khamis Ame-OMPR,ZNZ
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema jamii inapaswa
kuendelea kuheshimu jukumu la walimu lililowapa dhima ya kujikubalisha
kuitekeleza kazi ya Ualimu katika kuwafinyanga watoto ili kuwa na uwezo
wa kuongoza ustawi wa Taifa lao hapo baadae.
Balozi
Seif alieleza hayo hapo Ofini kwake Vuga Mjini Zanzibar katika hafla
fupi ya kuukabidhi Uongozi wa Skuli ya Msingi ya Uzini ya Wilaya ya Kati
mashine ya Fotokopi, Meza pamoja na Wino zake ili kusaidia machapisho
ya kazi za Skuli hiyo.
Makabidhiano
hayo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwaka 2011 wakati akiwa mgeni
rasmi kwenye sherehe za kuwazawadia Wanafunzi bora wa darasa la kumi na
Moja { Form 1V } wa Skuli hiyo.
Balozi
Seif alisema ufinyanzi wa Watoto kitabia, Kimaadili na Kitaaluma ni
kazi ya wito na ni ngumu ambayo inahitaji kuungwa mkono na jamii ili
iweze kutoa matunda bora ya ustawi wa jamii.
“
Mimi naelewa fika kwamba kazi ya ualimu ni nzito sana na inahitaji
subra kwani hata mimi niliwahi kuisomea na hatimae kuifanyia kazi ingawa
kwa kipindi kifupi “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi wa Skuli ya Msingi ya
Uzini kuhakikisha kwamba mashine hiyo ambayo ni hazina kwao wanaitumia
katika mazingira mazuri ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu ujao.
Aliwapongeza
walimu na wanafunzi wa Skuli hiyo kwa ustahamilivu wao wa muda
mrefu tokea kutolewa kwa ahadi hiyo ambayo ilichelewa kutokana na
mawazo yaliyochanganya kufikiria kwamba kilichokuwa kikihitajiwa katika
maombi ya skuli hiyo ni kompyuta kumbe ni Fotokopi.
Akitoa
shukrani kwa Niaba ya Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Uzini
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Skuli hiyo Tatu Ame Suleiman alisema msaada huo
wa Fotokopi umeleta Ukombozi kwao.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi Tatu alisema eneo kubwa la Uzini hadi Mchangani lilikuwa
likikosa huduma ya fotokopi jambo ambalo lilileta usumbufu hasa kwa
walimu na wanafunzi wakati wa vipindi vya Mitihani ya majaribio sambamba
na kazi za kila siku ya Kiutawala Skulini hapo.
“ Tunalazimika
kutoa shukrani za dhati kwao Mh. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa
msaada wako huu na furaha yetu ya kupata mashine hii tunaimani
itaenea eneo letu lote la Uzini na Mchangani yake “. Alionyesha furaha
yake Mwalimu Tatu Ame.
Naye
kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza Hassan alieleza
kwamba kitendo hicho cha msaada wa Mashine ya Fo tokopi mbali ya kuwa
cha Kihistoria bali pia kinaongeza ujirani mwema kati ya Wananchi wa
Jimbo la Uzini na wale wa Jimbo la Kitope linaloongozwa na Balozi Seif.
Mwakilishi
huyo wa Jimbo la Uzini aliushauri Uongozi wa Skuli hiyo kuandaa
utaratibu maalum utakaowezesha matumizi bora ya Mashine hiyo na kutoa
huduma pia kwa wananachi wengine wa kawaida katika eneo hilo.
Raza
alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi
Seif kwa umakini wake wa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama hicho
kilichopata ridhaa ya Wananchi walio wengi ya kuongoza Serikali.
Mashine hiyo ya Fotokopi, Meza na Wino zake imegharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 1,500,000/- .


0 comments:
Post a Comment