SERIKALI
ya Zanzibar imetangaza mpango wake wa kuibinafsisha Hoteli ya Bwawani kwa
wawekezaji wenye uwezo wa kuiendesha kibiashara katika mwaka huu wa fedha.
Mpango
huo umetangazwa jana mjini Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo, Said Ali Mbarouk, wakati alipokuwa akifunga mjadala wa bajeti yake
katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.
Hoteli
ya Bwawani ilianza kujengwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman
Karume, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na wapinga maendeleo mwaka 1972.
Waziri
Mbarouk alisema akipatikana mwekezaji makini atapatiwa kuendesha hoteli hiyo
ili ijiendeshe kibiashara na kukuza mapato ya sekta ya utalii Zanzibar.
Alibainisha
kuwa mpaka sasa haijafahamika hatima ya wafanyakazi wa Shirika la Utalii
Zanzibar (ZTC) wapatao 119 ambalo serikali imeamua kulivunja kuanzia mwaka huu.
Waziri
Mbarouk alisema serikali ipo katika hatua za kubinafsisha Hoteli ya Bwawani
ambayo sasa inakabiliwa na uchakavu mkubwa na kusababisha sehemu kubwa ya
hoteli hiyo kutotumika.
Waziri
Mbarouk alisema katika mwaka wa fedha 2012/13 ilikusanya sh milioni 826.9 na
ilitumia shilingi 817.9 sawa na asilimia 99 ya makusanyo ya mapato yake.
CHANZO TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment