Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
Mimba
za utotoni zimeelezwa kuwa ni kikwazo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa nchi
masikini ikiwemo Tanzania .
Akitoa
taarifa ya siku ya Idadi ya Watu Duniani leo mjini Zanzibar , kwa niaba ya
waziri wa Fedha wa SMZ Omari Yusufu Mzee, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar
Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini, amesema mimba hizo zimekuwa zikiathiri mipango
ya kimaendeleo kwa nchi masikini.
Amesema
Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi za bara la Afrika zenye idadi kubwa ya
wasichana wanaopata mimba za utotoni wakiwa shuleni na wale wasiosoma, imebaini
kuwa mamba hizo ni kikwazo katika mipango ya maendeleo ya uchumi mikoani.
Amesema
kwa mfano Zanzibar , wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wenye umri kati
ya miaka 12 na 18 wamekuwa wakiacha masomo kutokana na kupata mimba wakiwa
shuleni.
Amesema
nyingi ya mimba hizo zimekuwa zikipatikana pasipo matarajio na mipango kwa watoto
hao ambao wameingia katika kundi la wazazi ambapo amesema ni matokeo ya kuanza
ngono utotoni zisizo salama.
Dr.
Mwinyihadi amesema mimba za utotoni humkosesha mtoto wa kike elimu ya lazima na
kumdumaza kimaisha wa kuanza mapambano mapema ya kujitegemea binafsi kimaisha
na kuzorota kwa ukuaji wa kiuchumi kwa taifa.
Amesema
pamoja na taarifa za wasichana 8,000 kuacha shule kila mwaka hapa nchini kwa
mimba, lakini idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wasichana wanaoozeshwa na
wazazi wao kwa watu waliowafanyia ukatili wa kingono.
Amesema
katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2008 hadi 2012, wasichana 659 waliacha
masomo katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba ambapo kati ya hao, watoto 277
waliacha masomo kutokana na ujauzito na wengine 382 waliolewa wakiwa shuleni.
Hata
hivyo Dr. Mwinyihadi amesema ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto wa
kike, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha vituo vijulikanavyo kama Mkono
kwa Mkono katika mikoa ya Unguja na Pemba ambapo yeyote anayefanyiwa ukatili wa
kijinsia hutoa ripoti na hatua kuchukuliwa kwa mkosaji.
Amesema hatua hiyo
imewafumbua macho wananchi na hata kupunguza kwa kiasi kikubwa vitendo vya
unyanyasaji kwa mtoto wa kike visiwani humo.
0 comments:
Post a Comment