Jumla ya tani 22.521 za
karafuu zenye thamani ya shlingi milioni 315, 039,000 zimenunuliwa na Shirika
la Biashara la Taifa Zanzibar (ZCTC) Kisiwani Pemba katika kipindi cha wiki
moja tokea kufunguliwa kwa msimu wa ununuzi wa zao hilo.
Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Pemba Hemed Suleiman Abdalla amesema kuwa karafuu
hizo zimenunuliwa na Shirika katika vituo vyake vitatu vilivyopo maeneo ya mjini Wete, Mkoani na Caheke Chake.
Aidha amesema kuwa Shirika limetoa nafasi kwa masheha kutoa taarifa kwa Wakuu wa Wilaya wakati wanapohitaji kufunguliwa kwa vituo katika maeneo yao na baada ya taarifa hizo kufika ofisini watakuwa tayari kufungua vituo kwa ajili ya ununuzi wa karafuu.
Akizungumzia suala la magendo ya karafuu Hemed amesema kuwa Serikali haitakuwa na muhali juu yawatakaobainika kuhusika na vitendo hivyo, ambapo sheria itachukua mkondo wake.
Amesema kuwa ni vyema wananchi kuepukana na watu wa magendo na badala yake wawe tayari kutoa taarifa ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Amesisitiza kuwa kila mwananchi atakayepeleka karafuu zake kwenda kuuza katika shirika la ZCTC atapata asilimia 80 huku asilimia 20 inakwenda kwa Serikali ambazo zitatumika katika huduma mbali mbali za maendeleo.
Amesema kuwa Serikali imepandisha bei ya karafuu hadi 14,000 kwa kilo lengo ni kuboresha hali za maisha za wakulima na kuwataka wananchi kupeleka karafuu zilizosafi katika vituo kwa ajili ya kuuza.
Ameeleza kwamba baadhi ya wakulima wamekuwa wakichanganya karafuu na makonyo kwa lengo lakupada kilo nyingi na kwamba jambo hilo hawatalifumbia macho kwani watu hao wanasababisha sifa mbaya za karafuu ya Zanzibar.

0 comments:
Post a Comment