Busara Promotions ni Taasisi inayoandaa tamasha la muziki la Sauti
za Busara, ikishirikiana na bodi ya wadhamini, uongozi, wafanyakazi pamoja na
wageni kutoka sekta ya sanaa na utamaduni Tanzania waliokutana mwishoni mwa
wiki kupanga mikakati na mipango katika hoteli ya Bluebay Beach Resort iliyopo
Kiwengwa, Zanzibar ili kupitia mafanikio ya muongozo uliopita na kupanga
mikakati na shughuli ya miaka mitano ijayo.
Imedhaminiwa na mfuko wa Kiholanzi Hivos, Bluebay Beach Resort
Zanzibar na wawezeshaji kutoka PEN Kenya, timu nzima ya Busara Promotions
ilijumuika pamoja ili kuweza kupanga mwongozo mpya katika taasisi, ambayo
imejenga ubora na nguvu katika kutangaza utamaduni na muziki wa Afrika
Mashariki na kati, kitaifa na kimataifa kwa miaka kumi iliyopita.
Ingawa Taasisi inajulikana kwa uandaaji wa tamasha la muziki ambalo
hufanyika moja kwa mwaka lijulikanalo kwa jina la Sauti za Busara (Sounds of
Wisdom), Busara Promotions pia huhusika nyuma ya pazia katika sekta ya
muziki, kujenga thamani ya muziki duniani kote na kanda zote kwa ujumla,
kujenga ujuzi na kuwapatia nafasi wasanii na wanamuziki, wataalam wa
muziki,kuimarisha miundombinu na kujenga mitandao ya kikanda na kitaifa.
Mipango ya miaka mitano ijayo
ni kujenga mafanikio ya awali ya Busara Promotions pamoja na kutambulisha
mawazo mapya na miradi ikiwa ni pamoja na kuongeza shoo zaidi za utamaduni kwa
Taasisi kwa mwaka mzima.
Busara Promotions inatarajia
kuwa hai katika mashirikiano na wasanii na wataalam wa muziki na kazi, mafunzo
na nafasi katika mitandao pamoja na kuimalisha muonekano wa muziki wa Kiafrika
na maelezo katika mitandao.
Busara Promotions inapenda
kutangaza kuwa wakati wa majadiliano, Bodi ya wadhamini imechagua wanachama
wapya watatu kujiunga na bodi ya wadhanimi ambao ni: Ally Saleh, Mzanzibari ni
mwaandishi wa habari anaejulikana, aliwahi kufanya kazi na Busara Promotions
wakati wa Kongamano la Viongozi wa Utamaduni na ukuaji wa uchumi Zanzibar mwaka 2011 Novemba.
Aliongoza majadiliano hayo kwa wadau wa biashara, utalii na wadau wengine
wanaohusika katika taasisi za utamaduni katika kuleta faida kwa wazawa.
Julia Bishop, ni mshauri
mtaalam na mkurugenzi mwanzilishi wa Chama cha Wawekezeji sekta ya Utalii
Zanzibar (ZATI), kuleta kwake utaalam wake katika utalii na biashara katika
bodi ya wadhamini Busara Promotions. Verena Knippel amesaidia baadhi ya
watanzania katika ratiba ya TV na filamu. Amewahi kuishi na kufanya kazi
Zanzibar kwa muda wa miaka mingi baada ya hapo alihamia Dar es Salaam na
kujiunga na DFID kama mtaalam wa kusaidia bajeti. Wanachama hawa watatu wa bodi
ya wadhamini watasaidia kuiongoza Busara Promotions na kutimiza malengo ya
miaka ijayo, kwa kuchangia ujuzi wao mbali mbali na uzoefu wao katika timu.
Kwa wakati huo huo, Bodi ya wadhamini wawili ambao ni waanzilishi,
Hilda Kiel na Emerson Skeens, wamejiuzulu katika nafasi zao kama bodi ya
wadhamini na kuwa wanachama washauri wa Busara. Mwenyekiti wa Bodi, Simai
Mohammed Said, aliwashukuru kwa huduma zao za miaka mingi katika taasisi na
kuwapongeza kwa kuendelea kushiriki kuwa washauri.
Busara Promotions inaandaa toleo la 11 la tamasha la muziki la Sauti
za Busara, litakalo fanyika kuanzia tarehe 13 mpaka16 February 2014, Mji
Mkongwe, Zanzibar. Tamasha litashirikisha majina bora ya wasanii wa muziki wa
Kiafrika.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi mtendaji wa Busara
Promotions, Rebecca Corey, kupitia barua pepe ifuatayo: rebecca@busara.or.tz.
Shukrani za dhati
kwa Bluebay Beach Resort, Zanzibar na wadhamini wetu wa Sauti za Busara
2014: Royal Norwegian Embassy, Hivos, Goethe Institute, Memories of
Zanzibar, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., SMOLE II na
wahisani wetu wote

0 comments:
Post a Comment