Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar,
imekamata tani 205 za mchele mbovu na dawa zilizopitwa na muda kwa matumizi
binadamu.
Hayo yamebainishwa na Mrajisi wa
Bodi hiyo, Dkt. Burhan Simai, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Mnazi Mmoja wilaya ya mjini Unguja. Alisema kati ya tani hizo 205
mchele mbovu, tani 130 zimeingizwa nchini na kampuni ya UTS RICE kutoka
Pakistan na tani 75 zimeingizwa na kampuni ya Inter Link kutoka Kenya.
Dkt. Simai alisema kwamba bidhaa
hizo zilifanikiwa k u k ama twa kutokana na operesheni maalumu iliyofanywa na
Bodi hiyo hivi karibuni na kukamata tende tani 3.4 zilizotoka Dubai.
Akizungumza na waandishi wa habari alisema bidhaa zote hizo zinafanyiwa
utaratibu wa kuangamizwa na baadhi kurejeshwa zilizotoka kwa gharama za
wamiliki wa bidhaa husika
Sambamba na hilo alisema kuwa
kumejitokeza tabia kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa hawahifadhi
vyema bidhaa zao na matokeo yake kuharibika mapema.
Kuhusu uingizwaji wa dawa feki hapa nchini
Mrajisi huyo alisema kwamba wameweka mtandao maalumu wa kuweza kugundua dawa
hizo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika. Alisema kuwa wakati wa
kusimamia sheria umefika kwani wa fanyabiashara wengi wamekuwa wakifanya
udanganyifu kwa masilahi yao binafsi bila ya kujali afya za watumiaji.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment