Watu wawili wamekamatwa na silaha katika bandari ya Zanzibar wakati wakitokea Dar es Salaam. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema watu
hao walikamatwa na bastola aina ya cz 92 ikiwa na risasi nane wakati
wakitokea Dar es Salaam kwa boti ya Kilimanjaro 4.
Alisema baada ya wahatumiwa hao kuhojiwa walieleza kuwa ni wamiliki
halali wa silaha hiyo, lakini Kamanda huyo alisisitiza kuwa sheria ya
watu kumiliki silaha haitumiki Zanzibar.
Alisema watu hao watafikishwa mahakamani. Aliwataja kuwa ni Daudi Obeto Matiku (40) na Emanual Joseph Obeto (35).
Hatua hiyo imekuja baada ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali
Mussa, kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na
usalama ili kupambana na wahalifu.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment