Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pamoja na Uongozi wa Kampuni ya
Usafirishaji wa vyombo vya usafiri ya Be Forward. JP wakigonganisha
grasi kwa furaha wakati wa tafrija maalum ya kutimiza mwaka mmoja kwa
Kampuni hiyo.
Balozi
Seif Ali Iddi akikabidhi hati ya gari aina ya Toyota Passo 2004 kwa
mshirika wa Kampuni ya Usafirishaji wa vyombo vya usafiri ya Be Forward.
JP aliyebahatika kupata zawadi hiyo kwenye tafrija ya Be Forward. JP. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya
pamoja na washindi wa zawadi mbali mbali ziliztolewa na Kampuni ya Be
Forward. JP kwenye Tafrija ya kutimia mwaka mmoja wa Kampuni hiyo Nchini
Tanzania. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
*******************************
Watanzania
wanapaswa kuwacha woga na kuanza kujenga dhana ya kujaribu katika
kufikiria kuanzisha miradi tofauti ya kiuchumi itakayotoa fursa za
ajira hasa kwa vijana na kuwaongezea kipato chao ili kukidhi mahitaji
yao ya kimaisha.
Ushauri
huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi katika tafrija maalum ya kutimia mwaka mmoja tokea kuanza kutoa
huduma hapa nchini kwa Kampuni ya Kimataifa ya Usafirishaji wa vyombo
vya usafiri ya Be Forward. JP iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency Kilimanjaro iliyopo Mjini Dar es salaam.
Balozi
Seif alisema wapo baadhi ya watu na taasisi tofauti hapa nchini ambazo
zimekuwa na uwezo mkubwa wa kujiongezea mapato zaidi kwa kuanzisha
miradi ya kiuchumi lakini zinashindwa kufanya hivyo kwa kuhofia kupata
hasara.
Alisema
wakati umefika kwa taasisi hizo kuiga mfano wa makampuni na taasisi
nyengine za kigeni akatolea mfano zile za nchini Japani ili kuona
zinakwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo hivi sasa
ulimwenguni.
“
Kwa nini jamii yetu hasa wafanyakazi wa umma waendelee kuwa na hofu hii
wakielewa kwamba bila ya kujaribu hakutapatikana maendeleo yoyote yale
“. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliipongeza Kampuni hiyo ya
usafirishaji wa vyombo vya usafiri ya Be Forward. JP Tanzania kwa
mchango wake mkubwa katika kusaidia uchumi wa Tanzania.
Aliuomba
Uongozi wa Kampuni hiyo kufikiria wazo la kufungua tawi lake jengine
Visiwani Zanzibar ili kuona huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo
zinastawisha pande zote mbili ya Tanzania.
Akizungumzia
suala la usafirishaji na utoaji wa bidhaa na vyombo vya usafiri
Bandarini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameiomba Mamlaka ya Mapato
Tanzania { TRA } kuongeza nguvu za ziada katika kushughulikia utoaji wa
mizigo kwa wakati muwafaka.
Alisema
hatua hiyo itawarahisishia wananchi kutoa mizigo yao kwa haraka na
kuepuka kutozwa fedha nyingi wakati makosa yanapotokea hufanywa na
baadhi ya watendaji wa Taasisi zinazosimamia mapato.
“
Inafikia wakati wananchi hutozwa fedha nyingi na wakati mwengine
wakalazimika kulipia fidia kwa bidhaa na mizigo yao wanapotaka kutoa
bandarini. Unapochunguza ukweli mara nginyi makosa yanayotokezea
hayasababishwi na wao “. Alifafanua Balozi Seif.
Mapema
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafirishaji wa vyombo vya usafiri ya Be
Forward. JP Bwana Hironori Yamakawa alisema kampuni hiyo tayari
imeshasafirisha zaidi ya magari 4,000 kutokea Japan na kuingia Dar es
salaam hadi mwezi Oktoba mwaka huu.
Bwana
Yamakawa alisema taasisi yake iliyotoa ajira kwa zaidi ya wafanyakazi
300 wa Kitanzania imekuwa ikipata mafanikio makubwa kutokana na
ushirirkiano mkubwa uliopo kati ya uongozi wa Taasisi hiyo na wazawa.
Mkurugenzi
Mkuu huyo wa Kampuni ya usafirishaji wa vyombo vya usafiri ya Be
Forward. JP alielezea faraja yake kutokana na huduma zinazotolewa na
taasisi yake kwa kusafirisha vyombo vya usafiri kutoka Japani hadi
Tanzania.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tawi la Tanzania Isaac Mbinile amewapongeza
wafanyabiashara, Taasisi za Umma na zile binafsi kwa uwamuzi wao wa
kushirikiana na Kampuni hiyo ulioleta mafanikio makubwa.
Kampuni
ya Kimataifa ya usafirishaji wa vyombo vya usafiri Be Forward. JP
imekuwa ikitoa huduma za kusafirisha magari kati ya Japani hadi Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati.
Katika
Tafrija hiyo maalum ya kutimia kwa mwaka mmoja wa Be Forward. JP
iliyoambatana na muziki laini ilijumuisha pia utolewaji wa zawadi kwa
washirika na wateja wa Kampuni hiyo.
Zawadi hizo ni pamoja na vyombo vya mtandao wa mawasiliano ya Internet { Ipad }, Mipira na Pampu zake, T. Shirts, Vikombe vya chai pamoja na Gari ndogo aina ya Toyota Passo 2004.



0 comments:
Post a Comment