Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein
Alisema kuwa mfumo huo mpya utakuwa wa manufaa zaidi kwa nchi kwa kuwa sio tu kuwa unahimiza umakini katika kuweka na kupanga malengo lakini pia upimaji wa matokeo kwa kuzingatia nyenzo za bajeti zilivyotumika.
Akihitimisha kikao cha Kutathmini Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika jana Ikulu, Dk. Shein aliitaka Wizara hiyo kutayarisha mwongozo wa upimaji na uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ili kuwapo na mfumo mmoja wa taarifa za aina hiyo.
Aliitaka wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi ikiwamo suala la kudai risiti wanaponunua bidhaa madukani. “Liwe ni jambo la mara kwa mara kwa kuwa si rahisi kwa wananchi kubadilika mara moja. Wahimizeni wafanyabiashara kutoa risiti wanapofanya mauzo halikadhalika muwaelimishe wananchi kuomba risiti kila wanaponunua bidhaa” Dk. Shein alisema.
Aliongeza kuwa mtindo wa baadhi ya wafanyabiashara kuwapa wateja uchaguzi wa bei kwa kuwatoza bei ndogo kwa bidhaa bila ya risiti na bei kubwa kwa bidhaa zilizokatiwa risiti unaharibu uchumi wa nchi na unapaswa kukomeshwa.
Kwa upande wa zoezi la uhakiki mali za serikali Rais aliagiza taarifa ya awali ya tathmini iliyokwishafanywa kwa wizara tano iwasilishwe serikalini ili iweze kufahamu mwelekeo wa mali zake.
Akizungumza katika kikao hicho Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad alitoa rai kwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kufanya kazi ya ziada ya kutoa elimu kwa wananchi kisiwani Pemba kutumia huduma za kibenki.
Alisema kuwa hivi sasa wananchi wengi kisiwani humo wanapata fedha nyingi kufuatia malipo ya mauzo ya karafuu lakini fedha hizo nyingi kazijulikani zinakwenda wapi.
Naye mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia alizishauri Bodi ya Mapato Zanzibar (ZBR) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushirikiana katika kutoa elimu kwa mlipa kodi kwa kuwa taasisi hizo lengo lao ni moja.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara hiyo kwa mwaka uliopita, Katibu Mkuu Khamis Mussa Omar, alizitaja wizara hizo kuwa ni Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati pamoja na Wizara ya Fedha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wizara hizo kwa pamoja zina jumla ya mali 119,974 zenye thamani ya Sh. trilioni 1.4.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment