Wanachama wa MWAPE SACCOS wameunda kamati ya watu saba na kuipa
jukumu la kufuatilia wadaiwa sugu walioshindwa kurejesha mikopo ambayo inafikia
zaidi ya shilingi milioni 40.
Uamuzi wa kuunda kamati hiyo umefikiwa na wanachama wa Saccos hiyo
kwenye mkutano wa dharura uliofanyika kwenye ukumbi wa Jamhuri na kuhudhuriwa
na Mrajis wa Vya vya Ushirika Pemba Abdi Saleh wenye lengo la kutafuta njia ya
kurejeshwa kwa mikopo hiyo .
Kamati hiyo inapongozwa na mwenyekiti Juma Shaban Juma ambapo
Khamis Hamad Nassor ambayo imepewa jukumu la kukutana na wadaiwa sugu pamoja na
wadhamini wa wadaiwa hao.
Mapema akitoa taarifa ya fedha , Mhasibu wa Saccos hiyo Rashid
Said Nassor amesema kuwa kwa mujibu wa makubaliano mdaiwa anatakiwa kuwasilisha
deni lake kila tarehe 12 ya kila mwezi.
Ameeleza kwamba Saccos inatakiwa kurejesha shilingi milioni 14,
835,000 /= kila mwezi katika benki ya CRDB , baada yab kukopeshwa shilingi
milioni 300/= na hadi sasa wamefanikiwa kurejesha shilingi milioni
148,350,000/=.
Aidha amefahamisha kwamba hesabu hiyo ni ya marejesho 10 na wanatakiwa
kurejesha marejesho 13 ili kufikia marejesho hayo bado wanadeni la shilingi
milioni 44,505,000/=na kuongeza kuwa wana deni la shilingi milioni 151,650 ,000/=
bila ya faida.
Kwa upande wake Mrajis wa vyama vya Ushirika Pemba, Abdi Saleh
amewataka viongozi wa Saccos hiyo kuandaa utaratibu utaofanikisha
kurejeshwa kwa fedha za mikopo zilizoganda kwa wanachama .
Amesema kuwa MWAPE SACCOS ni moja ya Saccos ambazo malengo na
mwelekeo wake ni mzuri, hivyo haitakuwa jambo la busara kuona kuwa wanachama
wanashindwa kurejesha mikopo kwa wakati .
0 comments:
Post a Comment