Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Aidha
amesifu juhudi zinazochukuliwa na Sultan Qaboos wa Oman katika
kuisadia Zanzibar katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kitaaluma.
Amesema
ni jambo la kutia moyo kuona uhusiano na ushirikiano kati ya Oman na Zanzibar
unaendelea kuimarika siku hadi siku.
Amesema
mbali na uhusiano ya kiserikali, nchi hizo pia zina uhusiano wa kindugu ambao
hauwezi kusahauliwa, hali inayopelekea watu wengi wa Oman kuamua kuja Zanzibar
kwa ajili ya mapumziko wakati wa likizo zao.
Akizungumza
na Balozi mdogo wa Oman Sheikh Saleh Al-Hafidh, aliyefika Ofisini kwake
Migombani kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi, Maalim
Seif amesema uhusiano huyo utazidi kuimarishwa kwa maslahi ya pande zote mbili.
Amesifu
kazi nzuri iliyofanywa na balozi huyo katika kipindi kifupi cha miezi mitatu
alichofanya kazi Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kuratibu na kufanikisha kufanyika
kwa Tamasha la Kiislamu hapa nchini.
Amemtaka
Sheikh Saleh aendelee kuwa balozi wa kuitangaza Zanzibar nchini Oman na nchi
nyengine atakazokwenda kuzifanyia kazi.
Kwa
upande wake Balozi mdogo wa Oman Sheikh Saleh Al-Hafidh, ameishukuru Serikali
na wananchi wa Zanzibar kwa kumpa mashirikiano mazuri yaliyorahisisha
kutekeleza majukumu yake ya kikazi kwa ufanisi.
Amesema
ataendelea kushirkiana na Zanzibar wakati wowote licha ya kumaliza muda wake wa
utumishi hapa nchini
0 comments:
Post a Comment