Wakati
wabunge wakitaka posho ya vikao iongozwe kutoka Sh100,000 hadi
Sh300,000 kwa siku, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepandisha
posho kutoka Sh100,000 hadi 150,000 kuanzia mwaka huu.
Uchunguzi
umebaini viwango hivyo vya posho vimeanza kutumika tangu kupitishwa kwa
bajeti ya mwaka 2013/14, kila mjumbe analipwa kiwango hicho cha posho
licha ya mshahara wake.
Katibu
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Yahya Khamis Hamad
alithibitisha viwango hivyo vipya vya posho kuanza kutumia mbali na
mishahara yao na posho mbalimbali za jimbo kila mwezi.
Hamad
alisema nyongeza hiyo ya kikao imetokana na mapendekezo ya Kamati ya
Uongozi ya BLW, baadaye kuridhiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed
Shein.
Alisema
kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, kamati ya uongozi ina wajibu
wa kuangalia kila mwaka maslahi ya wawakilishi, lakini mwaka jana posho
za vikao hazikuangaliwa badala yake ziliangaliwa posho nyingine na
mishahara yao.
Mabadiliko ya posho ya vikao mishara na posho mbalimbali za wajumbe.
0 comments:
Post a Comment