Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesifu
maendeleo yaliyopatikana katika shule ya msingi ya ALI KHAMIS CAMP
inayosimamiwa na Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ).
Amesema shule hiyo imekuwa na maendeleo ya kupigiwa mfano kwa shule za
Tanzania, na kwamba yamepatikana kutokana na umakini na nia njema ya
jeshi hilo katika kuwapatia watoto elimu bora.
Maalim Seif ametoa pongezi hizo katika shule hiyo, wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za elimu kisiwani Pemba.
Aidha
amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na mashirikiano makubwa
yaliyopo kati ya wananchi, Wizara ya elimu pamoja na Jeshi hilo,
sambamba na nia njema iliyopo katika kuwapatia wananchi maendeleo.
Amesema
Jeshi la Wananchi ni taasisi muhimu katika kuchangia maendeleo ya nchi,
na kwamba vikosi vya (14 na 151 KJ) vimeonyesha mwitikio mzuri wa
kushirikiana na wananchi katika jitihada za kujikwamua kimaendeleo.
Amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuhakikisha kuwa
linatimiza malengo yake ya kuwapatia elimu pamoja na huduma za afya
wananchi wa eneo hilo.
Katika
ziara hiyo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ameahidi
kuchangia mifuko 50 ya saraji ndani ya kipindi cha wiki moja, ili
kuchangia ujenzi wa shule hiyo, sambamba na kugharamia mafuta
yatakayotumika kwa ajili ya usafishaji wa kiwanja cha michezo kwa watoto
katika eneo hilo.
Mapema Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo Eugene Anathory Ruta amesema mafanikio ya shule hiyo yamechangiwa
kwa kiasi kikubwa na ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais aliyoifanya
katika skuli hiyo mwezi Juni, mwaka huu.
Amesema
tangu kufanyika kwa ziara ya mwezi Juni, wafadhili kadhaa wamejitokeza
kuchangia maendeleo ya shule hiyo, na kwamba sasa wana mpango wa kujenga
shule za maandalizi na Sekondari ambazo tayari ujenzi wake umeanza
hatua za msingi.
Kwa
upande wake kamanda wa kikosi cha (14 KJ) J.K. Mbwelo amesema maendeleo
ya shule hiyo hailengi kwa wanajeshi pekee bali kwa jamii nzima
iliyowazunguka.
Kwa sasa wananchi wengi wa maeneo ya Machomanne, Wawi na Vitongoji wamekuwa wakipatiwa huduma za matibabu na elimu katika kituo cha afya ya shule katika kambi hiyo ya Ali Khamis Camp.
Kwa sasa wananchi wengi wa maeneo ya Machomanne, Wawi na Vitongoji wamekuwa wakipatiwa huduma za matibabu na elimu katika kituo cha afya ya shule katika kambi hiyo ya Ali Khamis Camp.
Maalim Seif pia alitembelea shule ya Sekondari ya Madungu na kuelezea kuridhishwa na maendeleo ya skuli hiyo.
Wakati
huo huo akiwa katika shule ya Fidel Castro, Makamu wa Kwanza wa Rais
amepongeza hatua ya kutengezwa na kujengwa upya kwa shule hiyo, hatua
ambao imeirejeshe hadhi yake ya asili.
Ameuagiza
uongozi wa shule hiyo kufanya kazi ya ziada, ili kuhakikisha kuwa ubora
wa majengo unakwenda sambamba na matokeo mazuri ya wanafunzi katika
mitihani ya Taifa.
Nae
Msaidi Mwalimu Mkuu wa shule ya Fidel Castro. Khamis Rashid Nassor,
amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa tayari wameweka mikakati
imara kuona kuwa shule hiyo inarejesha hadhi yake ya Kitaaluma.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa na
makamanda wa vikosi vya (14 na 151 KJ) wakati akiwasili katika kambi ya
jeshi ya Ali Khamis Camp Vitongoji, kuangalia maendeleo ya shule ya
msingi iliyo chini ya Jeshi hilo.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa na
makamanda wa vikosi vya (14 na 151 KJ) wakati akiwasili katika kambi ya
jeshi ya Ali Khamis Camp Vitongoji, kuangalia maendeleo ya skuli ya
msingi iliyo chini ya Jeshi hilo.
Matengenezo
hayo makubwa ya shule hiyo, nyumba za walimu na mabweni ya wanafunzi,
pamoja na ujenzi mpya wa jengo la utawala na vyumba vya kusomea,
yamegharimu zaidi ya shilingi Bilioni tatu na nusu.
Aidha
katika hali siyokuwa ya kawaida, Maalim Seif aliingia madarasani kuona
jinsi walimu wanavyofundisha pamoja na kuangalia ufahamu wa wanafunzi
katika shule za Madungu na Fidel Castro
CHANZO MZALENDO.
0 comments:
Post a Comment