Kumekuwa
na mtafaruk mkubwa leo hapa maeneo ya mjini na vitongoji vyake kufuatia
uamuzi wa Baraza na Mji la Zanzibar (ZMC) na SMZ yake kuamua kuondosha
kituo cha dala dala pale Darajani.
Wameyafanya haya bila kumshauri mtu, si wenye dala dala au wananchi watumiaji.
Yametangazwa
haya kupitia ‘press conference’. Mkurugenzi wa Baraza la Mji (ZMC)
Maalim Abeid Juma Kombo anaona inatosha kufanya hivyo. Wrong.Ilikuwa ZMC
wakutane na stakeholders na isiwe leo kwa kesho!
ZMC,
SMZ wanaona inatosha kuweka askari na bunduki pale Darajani kutisha
watu na kuwapiga watu wanaopita eti wanavunja ‘kanuni’. Uamuzi huu
umepata baraka zote za serikali, akiwemo Rais Shein, na CCM Zanzibar.
Uamuzi huu wanaona unawakomoa wenye daladala, na wenyewe wanasema
‘wapemba’…..hizi ndio sera zao.
Ukweli
hasa uamuzi huu unawasumbua sana wananchi wa Zanzibar, kuna walemavu,
kuna wazee wasiojiweza, kuna wanafunzi wa skuli (wengine tayari wameanza
kupotea) maana vituo vipya hawavijui, na in fact, havipo.
Uamuzi huu utaleta mvurugano mkubwa katika mji, uchafuzi wa mji, uvurugaji wa mipango miji.
Leo
Mkurugenzi Abeid na Waziri wake Haji Omar Kheir anadhani kuweka kituo
cha dala dala pale nyuma ya iliyokuwa baraza la wawakilishi la zamani,
ni sawa. This is wrong, tena wrong sana.
Inanishangaza
sana kuona uamuzi kama huu umefikiwa na aina ya watendaji tulionao leo,
wamesoma, wametembea na kuona mambo: lakini ujinga, na kutu katika
vichwa vyao umeganda, kama gundi.
Najua
kuwa uamuzi huu unalenga zaidi kuelekea uchaguzi wa 2015, mipango hii
inajulikana; ni mipango ya CCM na taasisi zake. Tayari kuna agenda
nyingi zinagusa kuelekea uchaguzi — kupandisha kodi za utoaji wa
makontena, kusajili wapiga kura feki (Pemba mpaka mtoto anayenyonya
anaandikishwa — ah ziara ya makamo wa pili wa riais hiyo, Pemba juzi).
na mengine mengi, kuajiri askari wengi wa vikosi hasa KMKM na baadaye
kuwafukuza kazi, na baadaye hawa hawa wanakuwa majambazi!!
Hili
na mengine yatajitokeza na tutayaona, lakini wanaoumia ni wananchi
wote. Hili la kuhamisha vituo vya dala dala, Dr.Shein liangalie upya Dr.
weeee; unachezewa akili na akina Abeid au kwa sababu jamaa yako wa
Chokochoko/Mkanyageni na Mjimbini? Haya twendeni hivyo hivyo kijamaa
jamaa na kujitegemea!
CHANZO;MZALENDO
0 comments:
Post a Comment