Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF)
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Alikabidhiwa fomu jana na Katibu wa Tawi hilo, Bakari Hamad Ali na aliwataka wanachama wa chama hicho kufanya kampeni za kistaarabu ambazo hazitaweza kumchafua mtu na kuleta makundi ndani ya chama hicho.
“Tuache makundi endapo tukigunduwa na kupata ushahidi kuwa mtu amewagawa wanachama kwa kutaka uongozi tutamnyang’anya nafasi hiyo na kufanya uchaguzi upya,” alisema Maalim Seif.
Kuchukuwa fomu kwa Maalim Seif kunafanya idadi ya watu watatu walioomba kuwania nafasi hiyo akiwamo Mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui na Mwenyekiti wa Tawi la Mtoni Kidatu A, Ali Juma Suleiman.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment