Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alifika Ikulu mjini Zanzibar jana kujitambulisha kwa Rais Shein baada ya kuteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.
Dk. Shein alimpongeza IGP Mangu kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao unampa jukumu kubwa la kuongoza jeshi hilo ambao wajibu wake wa kwanza ni kulinda usalama wa raia na mali zao.
Alimueleza IGP Mangu kuwa Jeshi la Polisi Zanzibar linashiriki vyema katika kuhami uchumi wa Zanzibar kwa kushirikiana na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na magendo ya karafuu na pia ulinzi katika maeneo mbalimbali ya hasa ya kitalii.
Dk. Shein alisema usalama katika sekta ya utalii ni kipaumbele cha kwanza kwa kuwa sekta hiyo kwa mujibu wa Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Zanzibar (Mkuza) ndio sekta kiongozi katika uchumi ambayo inaipatia Zanzibar asilimia 80 ya fedha za kigeni na kuchangaia aslimia 27 ya pato lake.
Kwa upande wake, IGP Mangu ambaye alikuwa amefuatana na Naibu Inspeta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame alimueleza Rais Shein kuwa jeshi lake limejipanga kutekeleza majukumu yake ikiwamo kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment