Home » » WAVUVI ZANZIBAR WAVUA SAMAKAI WA MAMILIONI NDANI YA MWEZI MMOJA

WAVUVI ZANZIBAR WAVUA SAMAKAI WA MAMILIONI NDANI YA MWEZI MMOJA

Jumla ya kilo 231,049 za Samaki aina mbali mbali wakiwa na thamani ya shilingi 549, 419, 000/= wamevuliwa  kwa kutumia vyombo vya uvuvi 338 vya wavuvi wa  Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu wa 2014.

Afisa Uvuvi Wilaya hiyo Bw Vuai Othman Haji amebainisha hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Kipangani Wete ambapo pia amefahamisha kwamba samaki aina ya Jodari na Nduaro ndiyo waliovuliwa kwa wingi .

Vuai amesema kuwa katika kipindi cha mwezi wa janauri samaki aina ya Jodari waliovuliwa ni 67,050  wakiwa na thamani ya shilingi 236,724,000 /= na Nduaro ni 56,214 wenye thamani ya 188,756,000 /= .

Aidha amefahamisha kwamba samaki aina ya kangaja , Vibua na Dagaa walifikia 45,268 wakiwa na thamani ya shilingi 39,672,800  huku samaki aina ya Pweza na Ngisi nao wakiwa ni 4,320 sawa na thamani ya shilingi 15,444,000 /=.

Naye mwenyekiti wa kamati za Wavuvi Wilaya hiyo  Bw Mohammed Kombo amesisitiza haja kwa wavuvi Wilayani humo kuendeleza ushirikiano na Idara ya Uvuvi ili kuifanya iweze kufamnikisha malengo yake ya kuyatunza mazingira ya bahari .

Hivyo Mwenyekiti huyo wa kamati za wavuvi Wilaya hiyo amesifu hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uvuvi kwa kushirikiana na kamati za Wavuvi katika kuwahasisha na kuwaalimisha wavuvi kufuata taratibu na sheria za uvuvi.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa