Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein jana amepokea rasmi Sarafu ya
Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko katika Viwanja vya
Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar-SUZA Kampasi ya Beit el Ras.
Hafla hiyo ambayo ilikwenda sambamba na ufunguzi
wa maonesho hayo ilishuhudiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif
Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ambao nao
walikabidhiwa sarafu hizo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa sarafu hiyo na
Naibu Gavana wa Benki Kuu, Juma Reli, Rais aliupongeza uamuzi wa Benki
Kuu wa kutoa sarafu hiyo maalum.
Alisema uamuzi huo ni wa kimaendeleo na kubainisha
kuwa yeye na viongozi wenzake wanathamini sana sarafu hiyo, hivyo
hawatakuwa tayari kuiuza hata kama thamani yake itapanda.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Gavana Juma
Reli alieleza kuwa kukabidhiwa kwa sarafu hiyo kwa Rais kunaashiria
uzinduzi rasmi wa uuzaji wa sarafu hiyo katika matawi yote ya Benki Kuu
nchini.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment