Katibu Mkuu wa Tume ya Utalii Zanzibar, Salehe Ramadhani
Ferouz, amesema mashambulizi ya baadhi ya watalii waliowahi kutembelea
visiwa vya Zanzibar, yameifanya picha ya kisiwa hicho cha amani
kubadilika.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mjini Zanzibar,
Ferouz alisema mashambulizi hayo yalikuwa mabaya na yalichafua mfumo
mzuri uliojengwa kwa kipindi kirefu katika visiwa hivyo, na kwamba
yamerudisha nyuma juhudi za tume ya kukuza utalii ndani ya Visiwa vya
Zanzibar.
“Kama tume, tuna wakati mgumu sana kwa sasa,
japokuwa wageni katika tamasha hili la Sauti za Busara wamekuwa ni
wengi, lakini tuna imani mwaka huu idadi ingekuwa kubwa zaidi, vitendo
hivi ndivyo vinatukwamisha,” alisema.
Kwa mujibu wa ofisa huyo wa utalii wa Zanzibar,
amesema kuwa wamekuwa wakikusanya wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali
duniani, tangu kuanzisha kwa tamasha hilo kwa mara ya kwanza miaka 11
iliyopita.
“Tunapata ahueni kubwa ya watalii wakati wa
tamasha hili linalochukua muda wa siku nne, hoteli zote hapa mjini
zimejaa, hii yote ni katika utalii wa muziki kwani wengi zaidi
wanapendelea kuja msimu huu kushuhudia tamasha la muziki wa asili,”
alisema Ferouz.
Kwa mujibu wa Ferouz, utalii ni sekta inayoongoza
katika kukuza uchumi Zanzibar kwnai inachangia asiliamia 25 ya Pato la
Taifa (GDP) na asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi za serikali.
Mwishoni mwa mwaka jana , Zanzibar ilikuwa
inakabiliwa na mashambulizi ya tindikali, ambayo wanawake wawili kutoka
Uingereza Katie Gee na Kirstie Trup, wote wakiwa na umri wa miaka 18,
wakati wakitembea katika njia ya sehemu ya zamani ya mji mkuu wa
Zanzibar, walimwagiwa tindikali na watu wawili waliokuwa wakiendesha
pikipiki.
Mashambulizi ya hivi karibuni yakiwamo ya upotevu
wa wanandoa wa Kifaransa ambao wanaaminiwa kwamba waliuawa na kutupwa
katika kisilinalozunguka nyumba yao.
Francois Cherer Robert Daniel na Brigette Mery
walionekana kwa mara ya mwisho mwaka jana. Taarifa kwamba wamepotea
zilianza kutangazwa Desemba 27 mwaka jana.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment