Jumuiya ya madereva Mkoa wa Kaskazini Pemba imetakiwa kuwaelimisha madereva na abiria kufuata sheria za usalama wa barabarani ili kupunguza ajali zinazosababishwa na gari za abiria .
Mkuu wa Wilaya ya Wete Omar Khamis Othman amesema kuwa bado ajali nyingi za barabarani zinazotokea husababishwa na madereva pamoja na abiria kutokana na kutozielewa vyema sheria za usalama wa barabarani .
Kauli hiyo ameitoa leo na wakati akifunga kikao cha kutathimini hali ya usafiri Mkoa wa Kaskazini Pemba kilichowashirikisha wadau wa usafiri kutoka asasi za kiraia, jeshi la polisi pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Miundo mbinu na mawasiliano Pemba.
Aidha wadau wa usafiri Mkoa huo ametathmini hali ya usafiri ilivyo hivi sasa na imeonekana kwamba baadhi ya madereva waneendelea kutotii sheria za barabarani ikiwemo kuendesha gari kwa mwendo wa kasi pamoja na kung'ing'iza abiria .
kutokana na hali hiyo imeagizwa kuwa alama wa barabarani ziwekwe ambazo zitasaidia madereva kutambua mwendo anaotakiwa aendshe gari katika sehemu husika hasa maeneo ya mijini na kwenye mikisanyiko ya watu .
Pamoja na hayo pia imeagizwa kwamba vyuma vlivyopo nyuma ya gari za abiria zionodhwe ili kuondoa tatizo la kupakia abiria wengi kupita uwezo wa gari zao.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment