Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge la Katiba kupitia Chama cha Allience for
Tanzania Farmers Party (AFP), Rashid Yussuf Mchenga amevuliwa uanachama
kwa madai ya kughushi saini ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaibu
Masoud Salum. Uamuzi huo ulitangazwa juzi na Mwenyekiti wa chama hicho
Taifa, Said Soud Said.
Said alisema saini hiyo aliyotumia kumhalalisha
katika ombi la barua yake iliyokwenda Ikulu ya Zanzibar, haikusainiwa na
Naibu Katibu Mkuu wa AFP Zanzibar na tayari wamefungua kesi Kituo cha
Polisi cha Madema.
Alisema majina yaliyotumwa Ikulu kwa uteuzi ni ya
Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Mohamed Rai aliyeteuliwa kuwa Mjumbe
wa Bunge la Katiba, Mahadhi Mohamed Mahadhi, (Soud) na mkewe Farida Juma
Khamis.
Naye Mchenga alisema chimbuko la kuibuliwa mgogoro
huo ni mwenyekiti na mkewe kukosa kwenye uteuzi huo na kwamba, hawezi
kughushi saini ya mtu.
“Ni wivu wa mwenyekiti wetu. Amechukia kutoteuliwa
yeye na mkewe. Hajui riziki ni mafungu saba, Bunge hili limemtoa udenda
na sasa anatapatapa tu mimi ni mjumbe halali,” alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
1 comments:
Wacheni uroho na uchu wa pesa! Kwani nyinyi mnakwenda kutumikia nchi au kutumikia matumbo yenu hata mugombane?
Post a Comment