Siku nne zimesalia kabla ya siku nne za kuandika historia
nyingine Visiwani Zanzibar kupitia onyesho kubwa la sanaa na muziki la
kimataifa linalotambulika kwa jina la Sauti za Busara.
Tamasha hilo lilianzishwa miaka 11 iliyopita na
kufanyika kila mwaka, linatarajiwa kuanza Februari 13 na kuhitimishwa
tarehe 16 ya mwezi huu.
Sauti za Busara ni tamasha linalowakutanisha
wasanii wa Kiafrika ili kuutangaza, kuhamasisha na kusherehekea
utamaduni wao bila kusahau wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani
ambao pia hufika kushuhudia na hata kushiriki.
Kupitia tamasha hilo wasanii hupata fursa ya
kujitangaza kimataifa wao binafsi au vikundi vyao hata kufanikiwa kuvuka
anga na kutambulika ndani na nje ya Bara la Afrika.
Baadhi ya wasanii waliofanikiwa kuvuka anga za
kimataifa kupitia Tamasha la Sauti za Busara ni pamoja na Jhikoman,
Abantu Mandingo, Mrisho Mpoto.
Hata hivyo, mbali ya kusherehekea utamaduni wa Kiafrika tamasha hilo lina faida nyingine zinazojitokeza kwa wasanii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Sauti za Busara,
Samia Mohamed anaeleza kuwa kila mwaka tamasha hilo limekuwa likitoa
ajira kwa zaidi ya Watanzania 150 jambo alilosema siyo rahisi kufikiriwa
au kufahamika na Watanzania wengi.
Mbali na ajira, Mohamed anasema kuwa tamasha hilo
pia limekuwa likikuza vipaji vya muziki kupitia kitengo chake
kijulikanacho kwa jila la ‘Busara extra’.
“Hatua hiyo inafanyika kwa kujumuisha matukio
mbalimbali ya maonyesho ambayo hutoa fursa kwa wasanii wa ndani
kuonyesha kazi zao binafsi,” anasema na kuongeza;
“Hatua hiyo imekuwa ikishawishi ongezeko la watalii wanaotembelea sehemu mbalimbali za utalii Visiwani Zanzibar.
Hali itakavyokuwa
Katika msimu wa Sauti za Busara, miji ya Zanzibar
hufurika wageni kutoka mataifa mbalimbali kutoka Afrika Mashariki,
Magharibi, Kaskazini, Kusini na nje ya bara hilo, huku biashara ya
utalii ikiongezeka kwa kasi.
Hadi sasa, mataifa mbalimbali duniani yameanza kuelekeza macho
na masikio yake Visiwani Zanzibar tayari kushuhudia tamasha hilo kwa
msimu wa mwaka huu 2014.
Baadhi ya shughuli zinazotarajiwa kutangulia mjini
Zanzibar katika uzinduzi wa tamasha hilo ni pamoja na maonyesho ya
filamu za Kiafrika, Kongamano la Wataalamu wa Filamu sanjari na paredi
maalumu siku ya ufunguzi wa Tamasha la Busara.
Mohamed anasema kuwa tamasha hilo halitakuwa na mgeni rasmi, badala yake Watanzania wote na Waafrika wote watahusika.
“Tangu tumeanza tamasha hili, miaka yote
hatujawahi kuwa na mgeni rasmi anayepewa kipaumbele tofauti na
Watanzania wenyewe lengo likiwa kutoa nafasi sawa ya kujionea fahari
ya tamasha hilo,” anasema.
Tofauti ya msimu huu
Mohamed anasema kuwa kwa mwaka huu tamasha hilo
linatarajiwa kuwa tofauti likilinganishwa na miaka iliyopita kutokana na
kuongezeka kwa maboresho mbalimbali ikiwamo ushiriki wa mataifa ya
Magharibi.
“Pia hata ubora wa wasanii watakaoshiriki,
ulinzi, ubora wa vyombo vya muziki pamoja na vitu vingine vingi,”
anasema Mohamed. Anabainisha kuwa pia Tamasha la Sauti za Busara msimu
huu litashuhudia uzinduzi wa mradi mpya ujulikanao kwa jina la ‘Santuri
safari’ ukiwa na dhamira ya kuangalia jukumu la MaDJ katika ukuzaji wa
muziki wa Afrika Mashariki.
“MaDJ waalikwa, wazalishaji wa muziki, watalaamu
wa sauti, waandaaji wa matamasha na wataalamu wa sanaa kutoka ukanda wa
Afrika watajumuika pamoja Zanzibar na kupata mafunzo hayo. Hiyo itakuwa
fursa muhimu katika kuangalia vitu vya kisasa,” anasema Mohamed.
Wasanii watakaoshiriki
Jumla ya vikundi 32 ndivyo vitakavyoshiriki Sauti
za Busara na kushambulia jukwaa ‘live’ vikichujwa kutoka vikundi 560
vilivyoomba kushiriki, huku 135 kati ya hivyo vikitoka Tanzania.
Baadhi ya vikundi na wasanii wataoshiriki ni
pamoja na Tausi Women’s Taarab (Zanzibar) Seven Survivor (Tanzania),
Baladna Taarab (Zanzibar) na Kundi la Jupiter, Okwess International
(DRC).
Wengine ni Dizu Plaatjies na The Ibuyambo Ensemble
( Africa Kusini), Addis Acoustic Project ft Melaku Belay (Ethiopia), OY
(Ghana), Switzerland Street Rat and Body Mind Soul (Malawi) na
Majestad Negra (Puerto Rico).
Hadi sasa, mataifa mbalimbali duniani yameanza kuelekeza macho
na masikio yake Visiwani Zanzibar tayari kushuhudia tamasha hilo kwa
msimu wa mwaka huu 2014.
Baadhi ya shughuli zinazotarajiwa kutangulia mjini
Zanzibar katika uzinduzi wa tamasha hilo ni pamoja na maonyesho ya
filamu za Kiafrika, Kongamano la Wataalamu wa Filamu sanjari na paredi
maalumu siku ya ufunguzi wa Tamasha la Busara.
Mohamed anasema kuwa tamasha hilo halitakuwa na mgeni rasmi, badala yake Watanzania wote na Waafrika wote watahusika.
“Tangu tumeanza tamasha hili, miaka yote
hatujawahi kuwa na mgeni rasmi anayepewa kipaumbele tofauti na
Watanzania wenyewe lengo likiwa kutoa nafasi sawa ya kujionea fahari
ya tamasha hilo,” anasema.
Wamo pia Jhikoman (Tanzania) Hoko Roro (Tanzania) Ashimba
(Tanzania, Finland) Swahili Vibes (Zanzibar), Tritonik (Mauritius) Joel
Sebunjo (Uganda), Abantu Mandingo (Tanzania), Segere Original
(Tanzania), Moyize (Rwanda) na Ricky na Marafiki (Kenya).
Tamasha bila Bi Kidude
Kwa mara kwanza tamasha hilo linafanyika bila
kuwepo kwa mwanamziki mkongwe na mashuhuri aliyeacha historia na heshima
kubwa ya kipekee, marehemu Bi Kidude.
Hata hivyo, Mohamed anasema kuwa hadi sasa
wamezungumza na Baraza la Sanaa Visiwani humo na taasisi mbalimbali kwa
ajili ya kuandaa mpango wa kumuenzi Bi Kidude.
“Suala hilo tumewaachia Baraza la Sanaa, ila sisi
tutabaki kama washauri kuhakikisha kunakuwa na hatua fulani ya kumuenzi
katika miaka yote aliyoshiriki katika muziki enzi za uhai wake,” anasema
Mohamed.
0 comments:
Post a Comment