Home » » Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia aagana na Balozi Iddi Seif Zanzibar

Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia aagana na Balozi Iddi Seif Zanzibar


Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Idd Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima alipokwenda kumtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Dkt. Mlima alikwenda kujitambulisha na kuwaaga viongozi wa Juu wa Kitaifa Zanzibar, na alikutana na Makamu wa Kwanza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Seif Shariff Hamad.
Dkt. Mlima aliteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia na makazi yake yatakuwa Kuala Lumpur.
Ubalozi huo wa Tanzania nchini Malaysia pia una jukumu la kuiwakilisha Tanzania katika nchi zifuatazo: Malaysia, Indonesia, Philipines, Thailand, Cambodia, Laos na Brunei.
Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Idd Seif akiongea  na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima alipokwenda kumtembelea Ofisini kwake Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa