Mkurugenzi
wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi CUF
Salum Bimani akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi yao, Vuga
Mjini Zanzibar.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Haki za
Binadamu wa CUF (hayupo pichani) Salum Bimani katika Ofisi ya Vuga,
Mjini Zanzibar.
=========== ======== ==========
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Chama
cha Wananchi (CUF) kimeilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
kutokana na jinsi ilivyosimamia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki
uliofanyika tarehe 2 mwezi huu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya CUF, Vuga Mjini Zanzibar leo,
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama hicho
Salim Bimani amesema Uchaguzi huo haukuwa huru na haukuwa wa haki.Amesema
vitendo vya kuvurugwa uchaguzi huo vilianza kujitokeza kuanzia wakati
wa kampeni na siku ya uchaguzi lakini pamoja na kutoa taarifa kwa Tume
ya Uchaguzi hakuna hatua yoyote iliyochukua.
‘’Chama
cha CUF kilibaini tokea mapema maandalizi ya fujo na matumizi mabaya ya
nguvu za dola pamoja na Vikosi vya Serikali, ambavyo viliandaliwa kwa
dhamira ya makusudi ya kuwapa haki wasiostahiki na pia kuwanyima watu
wengi haki yao ya kufanya maamuzi ya kidemokrasi’’, alisema Salim
Bimani. Aliongeza
kuwa upo ushahidi kwamba Vikosi vilitumika kuwalinda na kuwasafirisha
wapigakura mamluki kutoka sehemu nyengine kuja kupiga kura bila ya
hatua yopyote ya kisheria kuchukuliwa.
Bimani
alidai kuwa vikosi hivyo vilithubutu kuwatisha baadhi ya wananchi
waliopaza sauti kupinga mwenendo huo haramu wa uchaguzi. “
Wananchi na Chama cha Wananchi, CUF , walijenga matumaini makubwa ya
kuona Uchaguzi huru na wa haki ukifanyika katika zama hizi ambazo
Zanzibar inaongozwa na Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chini ya
misingi ya maradhiano ya kisiasa, inayozingatia amani, utulivu,
demokrasi na mshikamano kupitia siasa za kistaarabu’’, aliongeza
Mkurugenzi Bimani .
Alisema
kutokana na kasoro nyingi katika uchaguzi huo mdogo, CUF imekosa imani
na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Daftari la Kudumu la wapigakura
kutokana na kuchezewa na halipo kwa misingi ya kutekeleza demokrasia,
Haki na Uadilifu. Bimani
alirejea kauli ya Chama hicho kutaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) ivunjwe ili
kutoa fursa ya kupatikana Mamlaka nyengine huru itakayoweza kusimamia
Uchaguzi wa Haki na wa Kidemokrasia.
0 comments:
Post a Comment